Utakapo ulizwa: vipi inakuwa kumuamini Manabii na Mitume?
السؤال
Swali/ Utakapo ulizwa: vipi inakuwa kumuamini Manabii na Mitume?
الجواب
Jawabu/: Sema Ninaamini kwa mkato kwamba Mitume wote ni wanadamu, kwamba wao ni watu wema katika watoto wa Adamu na kwamba Mwenyezi Mungu amewachagua kwa ajili ya kufikisha sheria yake ambayo aliyo iteremsha kwa waja wake, Mitume hao wanawalingania wanadamu wamuabudu Mwenyezi Mungu mmoja ambae hana mshirika na kujiweka mbali na ushirikina na washirikina. na utume ni kuchaguliwa na Mwenyezi Mungu na haupatikani kwa kujitahidi wala kwa kufanya ibada nyingi, wala kwa kuwa mwema au akili nyingi, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mwenyezi Mungu anajua wapi aweke utume wake} (Al Anaam 124)
Na Nabii wa kwanza ni Adam amani ziwe juu yake, na Mtume wa kwanza ni Nuhu amani ziwe juu yake na Mtume wa mwisho na mbora wao ni Muhammad Bin Abdillah Mkurayshi katika koo ya banii hashim, sala na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao wote, na mwenye kukanusha Mtume atakuwa amekufuru na mwenye kudai utume baada ya Muhammad rehma na amani ziwe juu yake atakuwa ni kafiri mwenye kumkadhibisha Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu anasema: {Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Manabii...} (Al-Ahzab 40) na amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Hakuna Mtume baada yangu).