Skip to content

Utakapo ulizwa: vipi inakuwa kuamini vitabu vilivyo shushwa?

السؤال

Swali/ Utakapo ulizwa: vipi inakuwa kuamini vitabu vilivyo shushwa?

الجواب

Jawabu/ Sema: Ni kuakinisha na kushahidilia kuwa Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ameshusha juu ya manabii wake rehma na amani ziwe juu yao vitabu na ametaja miongoni mwa vitabu hivyo ni: Kurasa za Ibrahim Tawrati Injili Zaburi na Qur'an, akashusha Kurasa za Ibrahim kwa nabii Ibrahim na Tawrat kwa nabii Musa na Injiri kwa nabii Issa na Zaburi kwa nabii Daud na Qur'an kwa nabi Muhammad Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao wote.

Na kitabu bora ni Qur'an ambacho ni maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, aliyasema kwa hakika wa matamshi yake na maana yake kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na akamsikilizisha Jibril amani ziwe juu yake, kisha akamuamrisha kuyafikisha kwa Mtume Muhammad rehmana na amani ziwe juu yake, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Imeteremshwa na Malaika mwaminifu} (Shuaraa 193) na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: { Hakika Sisi tumekuteremshia Qur'ani kidogo kidogo} (Al Insan 23) na kauli ya Mwenyezi Mungu mtukufu: { mpe ulinzi apate kusikia maneno ya Mwenyezi Mungu} (Tawba 6)

Na hakika Allah ameihifadhi Qur'an kutokana na kupotoshwa kuzidishwa na kupunguzwa na kitabu hicho kimehifadhiwa katika vitabu na vifua mpaka Mwenyezi Mungu atakapo zichukua roho za waumini kabla ya kusimama kiyama katika zama za mwisho, atakinyanyua kitabu hicho kwake na hakutabaki chochote katika Qur'an.