Utakapo ulizwa: vipi inakuwa kumuamini Malaika wa Mwenyezi Mungu Mtukufu?
السؤال
Swali/ Utakapo ulizwa: vipi inakuwa kumuamini Malaika wa Mwenyezi Mungu Mtukufu?
الجواب
Jawabu/ Sema: Ni kusadikisha na kuamini kwa mkato juu ya kuwepo kwa Malaika na sifa zao na uwezo wao na kazi zao na yale wanayo amrishwa, na kwamba wao ni viumbe vya Allah vitukufu vikubwa Allah ameviumba kutokana na Nuru, Amesema Allah Mtukufu: {Hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayo waamrisha na wanatenda wanayo amrishwa} (Attahriim 6) na wana mbawa mbili na tatu na nne na zaidi ya mbawa hizo na idadi yao ni kubwa mno na hakuna anae jua idadi yao ila ni Allah Mtukufu. na akawakalifisha Mwenyezi Mungu kwa majukumu makubwa, miongoni mwao kuna walio beba Arshi na kuna walio wakilishwa kwa ajili ya vizazi na kuna wanao hifadhi matendo ya viumbe na kuna wanao hifadhi viumbe na kuna walinzi wa pepo na moto na majukumu mengine na mbora wa malaika ni Jibril -amani ziwe juu yake- na yeye amekalifishwa na kazi ya kushusha wahyi (Ufunuo) kwa Mitume. tunapaswa kuamini kuwepo kwa malaika kwa jumla na kwa upambanuzi kama alivyo tueleza Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kitabu chake na katika sunnahh za Mtume rehma na amani ziwe juu yake na mwenye kukanusha kuwepo kwa malaika au akadai kuwa uhakika wa malaika uko tofauti na alivyo eleza Mwenyezi Mungu Mtukufu basi mtu huyo anakuwa kafiri kwa kukadhibisha kwake habari ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na habari ya Mtume rehma na amani ziwe juu yake,