Utakapo ulizwa ni zipi nguzo za Imani?
السؤال
Swali/ Utakapo ulizwa ni zipi nguzo za Imani?
الجواب
Jawabu/ Nguzo za imani ni sita nazo: Ni kumuamini Mwenyezi Mungu na Malaika wake na Vitabu vyake na Mitume wake na Siku ya mwisho na kuamini Qadar ya Kheri za Allah na Shari zote zinatokana na Mwenyezi Mungu mtukufu
Na haitimii imani ya mtu ispokuwa atakapo amini mambo hayo yoote kwa namna ambayo Qur'an na sunnahh za Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake zimeelekeza na mwenye kukanusha moja katika hayo atakuwa ametoka katika Uislam na ushahidi wa hayo ni kauli ya Allah Mtukufu: {Sio wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi. Bali wema ni wa anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii na anawapa mali, kwa kupenda kwake, jamaa na mayatima na masikini na wasafiri na waombao na katika ukombozi na akawa anashika Sala na akatoa Zaka na wanao timiza ahadi yao wanapo ahidi na wanao vumilia katika shida na dhiki na wakati wa vita; hao ndio walio sadikisha na hao ndio wajilindao.} (Albaqaraa 177) na kauli ya Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake wakati alipo ulizwa kuhusu Imani, alisema: (Ni kumuamini Mwenezi Mungu na Malaika wake na Vitabu vyake na Mitume wake na Kuamini siku ya mwisho na kuamini Qadar ya Allah ya heri zake na shari zake) Imepokelewa na Imamu Muslim.