Skip to content

Utakapo ulizwa ni ipi dini yako?

السؤال

Swali/ Utakapo ulizwa ni ipi dini yako?

الجواب

Jawabu/ Sema: Dini yangu ni Uislam na maana ya Uislam ni kujisalimisha kwa Allah kwa kumpwekesha na kunyenyekea kwake kwa kumtii Allah na kujiweka mbali na Ushirikina na washiriina, kama alivyo sema Allah Mtukufu: (Hakika dini inayo kubaliwa kwa Allah ni Uislam) Al-Imran 19. na amesema Allah Mtukufu: (Na anaye tafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye akhera atakuwa katika wenye kukhasiri) Al-Imran 85. Mwenyezi Mungu hakubali dini isiyokuwa dini yake ambayo alimtuma Mtume wake Muhammad rehma na amani za Allah ziwe juu yake, kwa sababu ndio iliyo futa sheria zote zilizo tangulia na yeyote mwenye kufuata dini usio kuwa Uislam huyo atakuwa amepotea njia ya uongofu na akhera atakuwa miongoni mwa watu wenye hasara watakao ingia katika jahanam na ubaya ulioje wa mafikio yake