Skip to content

Utakapo ulizwa ni kwa kitu gani umemjua Mola wako mlezi?

السؤال

Swali/ Utakapo ulizwa ni kwa kitu gani umemjua Mola wako mlezi?

الجواب

Jawabu/ Sema: Nimemjua kwa maumbile ambayo aliyo niumba nayo ya kumjua na kukiri kimaumbile kwa kuwepo yeye Mwenyezi Mungu na kumtukuza na kumuogopa yeye, kama nilivyo mjua kwa kutizama na kuzingatia katika dalili zake na viumbe vyake, kama alivyo sema Allah Mtukufu: {Miongoni mwa dalili zake ni usiku na mchana na jua na mwezi} surat Fuswilah, viumbe hivyo vimeumbwa kwa mpangilio wake na umakini na uzuri haviwezi kujipatisha vyenyewe lazima viwe na muumbaji alie viweka baada ya kuwa havipo na viumbe hivyo ni hoja za mkato juu ya kuwepo kwa aliye viumba mwenye uwezo mkubwa na mwenye hekima, viumbe vyote vina kiri kuwepo muumbaji wao na Mfalme wao na mwenye kuwapa rizki na mwenye kuwapangilia mambo ya rizki zako na mambo yao ispokuwa watu wachache ambao hawa kiri hivyo, Miongoni mwa viumbe vyake: Mbingu saba na Ardhi saba na vilivyomo katia viumbe ambavyo hakuna yeyote anae jua idadi yake na uhakika wake na hali za viumbe hivyo ila ni Allah na hakuna anae vilea na kuviruzuku ila ni Allah aliye hai na mwenye kusimamia mambo yote mwenye uwezo wa kuumba na mwenye sifa ya ukubwa, anasema Allah mtukufu: {Hakika Mola Mlezi wenu ni Mwenyezi Mungu aliye ziumba mbingu na Ardhi katika siku sita. Kisha akatawala juu ya Kiti cha Enzi. Huufunika usiku kwa mchana, ufuatao upesi upesi. Na jua na mwezi na nyota zinazo tumika kwa amri yake. Fahamuni! Kuumba na amri ni zake. Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote} Al-A'raaf 54