Skip to content

Birika langu ukubwa wake ni sawa na mwendo wa mwezi mzima, maji yake ni meupe kuliko maziwa, na harufu yake ni nzuri kuliko ya Miski

Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Amrou -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:

"Birika langu ukubwa wake ni sawa na mwendo wa mwezi mzima, maji yake ni meupe kuliko maziwa, na harufu yake ni nzuri kuliko ya Miski, Vikombe vyake ni kama idadi ya nyota za mbinguni, yeyote atakaye kunywa kwenye birika hilo hatopatwa na kiu milele"

«حَوْضِي مَسِيرَةُ شَهْرٍ، مَاؤُهُ أَبْيَضُ مِنَ اللَّبَنِ، وَرِيحُهُ أَطْيَبُ مِنَ المِسْكِ، وَكِيزَانُهُ كَنُجُومِ السَّمَاءِ، مَنْ شَرِبَ مِنْهَا فَلاَ يَظْمَأُ أَبَدًا».

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Ufafanuzi

Ametoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yeye atakuwa na Birika siku ya Kiyama urefu wa Birika hilo ni sawa na mwendo wa miguu wa mwezi mzima, na upana wake hivyo hivyo, Na kuwa maji yake ni meupe kulio maziwa, Na kuwa harufu yake ni nzuri kuliko harufu ya Miski, Na Mabirika yake ni mfano wa nyota za mbinguni kwa wingi wake, Atakaye kunywa katika Mabirika hayo hatopatwa na kiu milele.

Maana ya Maneno

...:

Katika Faida za Hadithi

Birika la Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mkusanyiko mkubwa wa maji wanaokwenda kunywa humo waislamu miongoni mwa watu wa umma wake siku ya kiyama.

Kupata neema kwa mwenye kunywa katika Birika na kwa hivyo hatopata kiu milele.

Rejea

Swahiih Al Bukhaariy (8/ 119) (6579).

Swahiih Muslim (4/ 1793) (2292).

Zaidi (4)

المفهم (6/91).

فتح الباري (11/472).

التنوير شرح الجامع الصغير (5/387).

فتح المنعم شرح صحيح مسلم (9/125).