Sema: Allaahumma kfinii bihalaalika an haraamika, wa aghninii bifadhlika amman siwaaka". Tafsiri: Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze kwa halali yako dhidi ya haramu yako, na unitajirishe kwa fadhila zako nisimuhitaji yeyote asiyekuwa wewe
Kutoka kwa Ally radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba mtu mmoja aliyeandikishana kujitoa katika utumwa alimjia akasema: Hakika mimi nimeshindwa kulipa deni tuliloandikishana, basi naomba unisaidie, akasema: Je, nikufundishe maneno ambayo alinifundisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hata kungekuwa juu yako na deni zito mfano wa mlima Swiri Mwenyezi Mungu atakulipia, akasema:
"Sema: Allaahumma kfinii bihalaalika an haraamika, wa aghninii bifadhlika amman siwaaka". Tafsiri: Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze kwa halali yako dhidi ya haramu yako, na unitajirishe kwa fadhila zako nisimuhitaji yeyote asiyekuwa wewe.
«قُلْ: اللَّهُمَّ اكْفِنِي بِحَلاَلِكَ عَنْ حَرَامِكَ، وَأَغْنِنِي بِفَضْلِكَ عَمَّنْ سِوَاكَ».
Alimuijia kiongozi wa waumini Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yake bwana mmoja mtumwa alikuwa kaandikishana na bwana yake na amekubaliana naye ili aikomboe nafsi yake na aiache huru ili awe huru, na hakuwa na mali, akasema: Hakika mimi nimeshindwa kulipa deni hilo juu yangu, nakuomba unisaidie kulilipa kwa mali, au kwa kunifundisha na kunielekeza, akasema kumwambia kiongozi wa waumini: Je, nikufundishe maneno aliyonifundisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake, lau kama ungelikuwa na deni mfano wa mlima Swiri wa kabila la Twayyi basi Mwenyezi Mungu angelikulipia kwa mstahiki wake, na angelikuokoa kutoka katika madhila yake, akasema: Sema: "Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze" na uniepushe na uniweke mbali "kwa halali yako" nitosheke nayo "dhidi ya" kutumbukia katika "haramu yako", na unitosheleze "kwa fadhila zako" na ukarimu wako "kutomuhitaji yeyote" katika viumbe.
Kuomba ushauri na kutaka rai ya wasomi wa dini.
Ni juu ya wasomi na walimu wa dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwapa muongozo walinganiaji, na kuwaelekeza katika yale yanayoweza kuwasaidia kwa yale yanayowatokea miongoni mwa matatizo.
Himizo la kumsaidia mwenye mkataba.
Himizo la kujifunza dua hii, na kumuomba Allah kupitia dua hii.
Riziki ya halali hata ikiwa ndogo, ni bora kuliko mali ya haramu hata ikiwa nyingi.
Kutosheka na Mwenyezi Mungu na kuwaacha viumbe.
Himizo la kumjibu muombaji kwa majibu mazuri ikiwa huna cha kumpa.
Sunanu Tirmidhiy (5/ 526) (3563).
Zaidi (9)
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين.
لسليم الهلالي (2/ 565).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين.
لمجموعة من الباحثين (2/ 1013).
كنوز رياض الصالحين.
لمجموعة من الباحثين (17/ 456).
فيض القدير شرح الجامع الصغير.
للمناوي (3/ 111).
النهاية في غريب الحديث والأثر (3/ 9).
Imenukuliwa katika vitabu
11 Vitabu- UCHAMBUZI NA UFAFANUZI WA MASUALA MENGI YA HIJA, UMRA NA ZIARA KWA MUJIBU WA MUONGOZO WA QUR'ANI NA SUNNAالتحقيق والإيضاح لكثير من مسائل الحج والعمرة والزيارة - النسخة المعتمدة* Allāhumma ikfini bihalālika ‘an harāmik waghnini bifadhlika ‘amman siwāka: (Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze kwa halali yako dhidi ya haramu yako, na unitajirishe kwa fadhila zako nisimhitaji yeyote asiyekuwa Wewe). ([93])
- Hisnu Al-Muslim Kutoka Katika Nyiradi Za Kitabu Na Sunnaحصن المسلم"Tafsiri: Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze kwa halali yako dhidi ya haramu yako, na unitajirishe kwa fadhila zako nisimuhitaji yeyote asiyekuwa Wewe."[177]
- Hisnu Al-Muslim Kutoka Katika Nyiradi Za Kitabu Na Sunnaحصن المسلمAllahumma ikfini bihalalika an haramika, wa aghnini bifadhlika amman siwak.
Zaidi (8)
- أدعية جامعةأدعية جامعة (للحرمين)53. «اللَّهُمَّ اكْفِنِي بِحَلالِكَ عَنْ حَرَامِكَ، وَأَغْنِنِي بِفَضْلِكَ عَمَّنْ سِوَاكَ».
- الذكر والدعاء والعلاج بالرقي من الكتاب والسنة"اللهم اكفني بحلالك عن حرامك، واغنني بفضلك عن سواك".
- المختصر في آداب السفر وصفة الحج والعمرة وآداب الزيارة والأدعية الجامعة مع ملحق بالفتاوى والمخالفات4- أدعية جامعة (للحرمين)«اللَّهُمَّ اكْفِنِي بِحَلالِكَ عَنْ حَرَامِكَ، وَأَغْنِنِي بِفَضْلِكَ عَمَّنْ سِوَاكَ».
- رياض الصالحينرياض الصالحين مع فوائد وهدايات - 7«اللهم اكْفِنِي بحلالك عَنْ حرامِكَ، وأغْنِنِي بفضِلكَ عمَّنْ سواكَ».
- قاموس الكبائر موسوعة الكبائر - المجموعة الأولى«اللَّهُمَّ اكْفِنِي بِحَلَالِكَ عَنْ حَرَامِكَ، وَأَغْنِنِي بِفَضْلِكَ عَمَّنْ سِوَاكَ» [94].
- قاموس الكبائر موسوعة الكبائر - المجموعة الأولى«اللَّهُمَّ اكْفِنِي بِحَلَالِكَ عَنْ حَرَامِكَ، وَأَغْنِنِي بِفَضْلِكَ عَمَّنْ سِوَاكَ» [115].
- قاموس الكبائر«اللَّهُمَّ اكْفِنِي بِحَلَالِكَ عَنْ حَرَامِكَ، وَأَغْنِنِي بِفَضْلِكَ عَمَّنْ سِوَاكَ» [94].
- قاموس الكبائر«اللَّهُمَّ اكْفِنِي بِحَلَالِكَ عَنْ حَرَامِكَ، وَأَغْنِنِي بِفَضْلِكَ عَمَّنْ سِوَاكَ» [115].