Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitusomesha Qur'ani katika kila hali madamu hana janaba
Kutoka kwa Ally radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitusomesha Qur'ani katika kila hali madamu hana janaba.
كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُقْرِئُنَا القُرْآنَ عَلَى كُلِّ حَالٍ مَا لَمْ يَكُنْ جُنُبًا.
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwafundisha Maswahaba zake Qur'ani na akiwasomesha yeye mwenyewe katika hali zote madam hajawa katika hali ya janaba litokanalo na tendo la ndoa kwa wakeze.
Kutofaa kusoma Qur'ani kwa mwenye janaba mpaka aoge.
Kufundisha kwa vitendo.
Sunanu Tirmidhiy (1/ 214) (146).
Sunanu Abii Daud (1/ 164) (229).
Sunanu Al Nasaai (1/ 144) (265).
Sunanu Ibn Maajah (1/ 375) (594).
Musnad wa Ahmad (2/ 61) (627).
Zaidi (1)
النهاية في غريب الحديث والأثر (917-167).