Skip to content

Hakika Allah humridhia mja anapokula chakula akamshukuru juu ya chakula hicho, au akanywa kinywaji chochote akamshukuru kwa kinywaji hicho

Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maliki -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake:

"Hakika Allah humridhia mja anapokula chakula akamshukuru juu ya chakula hicho, au akanywa kinywaji chochote akamshukuru kwa kinywaji hicho".

«إِنَّ اللهَ لَيَرْضَى عَنِ الْعَبْدِ أَنْ يَأْكُلَ الْأَكْلَةَ فَيَحْمَدَهُ عَلَيْهَا، أَوْ يَشْرَبَ الشَّرْبَةَ فَيَحْمَدَهُ عَلَيْهَا».

Imepokelewa Imamu Muslim
Sahihi
Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa shukurani za mja kwa Mola wake Mlezi juu ya fadhila zake na neema zake ni miongoni mwa mambo ambayo huleta radhi za Allah; akala chakula akasema: Al-hamdulillah, na akanywa kinywaji na akasema: Al-hamdulillah.

Maana ya Maneno

...:

Katika Faida za Hadithi

Ukarimu wa Allah Mtukufu, ametoa fadhila zake kwa riziki na kisha akaridhia shukurani.

Radhi za Allah hupatikana kwa sababu nyepesi, kama kushukuru baada ya kula na kunywa.

Katika adabu za chakula na kinywaji: Ni kumshukuru Allah Mtukufu baada ya kula na kunywa.

Rejea

Swahiih Muslim (4/ 2095) (2734).

Zaidi (10)

نزهة المتقين شرح رياض الصالحين.

لمصطفى الخن وغيره (1/ 164).

بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين.

لسليم الهلالي (1/ 215).

شرح رياض الصالحين من كلام سيد المرسلين.

لابن عثيمين (2/ 203).

كنوز رياض الصالحين.

لمجموعة من الباحثين.

تطرز رياض الصالحين.

لفيصل آل مبارك (ص764).