Skip to content
Orodha ya Sura /

التغَابُن

التغَابُن is chapter 64 of the Quran and has 18 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

18 Aya Sura Na. 64
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

يُسَبِّحُ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۖ لَهُ ٱلۡمُلۡكُ وَلَهُ ٱلۡحَمۡدُۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ

Kinamtakasa Mwenyezi Mungu kila kilichomo katika mbingu na katika ardhi. Ufalme ni wake, na sifa njema ni zake. Na Yeye ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.

Explanation & meanings · 1
  1. Vitu vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi vinamtakasa Mwenyezi Mungu na kila kisicho kuwa laiki na utukufu wake. Yeye ndiye peke yake Mwenye ufalme ulio timia, na Mwenye sifa njema, na ndiye Mwenye uweza ulio timia juu ya kila kitu.

هُوَ ٱلَّذِي خَلَقَكُمۡ فَمِنكُمۡ كَافِرٞ وَمِنكُم مُّؤۡمِنٞۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٌ

Yeye ndiye aliye kuumbeni. Miongoni mwenu yupo aliye kafiri, na yupo aliye Muumini. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda.

Explanation & meanings · 1
  1. Yeye peke yake ndiye aliye kuumbeni mlipo kuwa si chochote. Basi kati yenu yupo anaye kanya Ungu wake, na miongoni mwenu yupo anaye sadiki. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda, na atakulipeni kwa mujibu wa vitendo vyenu.

خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّ وَصَوَّرَكُمۡ فَأَحۡسَنَ صُوَرَكُمۡۖ وَإِلَيۡهِ ٱلۡمَصِيرُ

Ameziumba mbingu na ardhi kwa haki, na akakupeni sura, na akazifanya nzuri sura zenu. Na marudio ni kwake.

Explanation & meanings · 1
  1. Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu na ardhi kwa hikima isiyo na ukomo, na akakuumbeni kwa sura, na akazifanya nzuri sura zenu, kwa kuwa amewafanya wanaadamu ndio viumbe walio nyooka vizuri. Na kwake Yeye ndiyo marejeo Siku ya Kiyama.

يَعۡلَمُ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَيَعۡلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا تُعۡلِنُونَۚ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ

Anajua viliomo katika mbingu na ardhi, na anajua mnayo yaficha na mnayo yatangaza. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliomo vifuani.

Explanation & meanings · 1
  1. Yeye Mwenyezi Mungu anajua yote yaliomo katika mbingu na ardhi, na anayajua mnayo yaficha, na mnayo yaeneza, ikiwa maneno au vitendo. Na Mwenyezi Mungu ametimia ujuzi wake kwa mnayo dhamiria katika nyoyo zenu.

أَلَمۡ يَأۡتِكُمۡ نَبَؤُاْ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن قَبۡلُ فَذَاقُواْ وَبَالَ أَمۡرِهِمۡ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ

Kwani haikukujieni khabari ya walio kufuru kabla, wakaonja matokeo mabaya ya mambo yao? Na wao wana adhabu iliyo chungu.

Explanation & meanings · 1
  1. Zimekwisha wafikieni khabari za walio kufuru kabla yenu, na wao wakameza ubaya wa matokeo wa mambo yao katika dunia. Na Akhera watapata adhabu yenye machungu makali.