Skip to content
الأنعَام /

Aya 92

6 : 92

Aya 92 of الأنعَام (6 : 92). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأنعَام Aya 165
Sura · الأنعَام
Kiswahili · Barawani
6 : 92

وَهَٰذَا كِتَٰبٌ أَنزَلۡنَٰهُ مُبَارَكٞ مُّصَدِّقُ ٱلَّذِي بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَلِتُنذِرَ أُمَّ ٱلۡقُرَىٰ وَمَنۡ حَوۡلَهَاۚ وَٱلَّذِينَ يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ يُؤۡمِنُونَ بِهِۦۖ وَهُمۡ عَلَىٰ صَلَاتِهِمۡ يُحَافِظُونَ

Na hiki ni Kitabu tulicho kiteremsha, kilicho barikiwa, chenye kuhakikisha yaliyo tangulia, na ili uuwonye Mama wa Miji na walio pembezoni mwake. Na wenye kuamini Akhera wanakiamini hichi, nao wanazihifadhi Sala zao.

Explanation & meanings · 1
  1. Na hii Qur'ani tumeiteremsha - kama tulivyo iteremsha Taurati - ina kheri nyingi, na itabaki mpaka Siku ya Kiyama. Inasadikisha Vitabu vilivyo teremshwa mbele yake, inaeleza khabari ya kuteremkwa kwao, ili iwape bishara Waumini, na iwakhofishe makafiri wa Makka na pembezoni mwake pande zote za dunia juu ya ghababu ya Mwenyezi Mungu, ikiwa hawakuifuata. Na wale wanao isadiki Siku ya malipo, kule kutaraji kwao thawabu na kukhofu adhabu, kunawapelekea kuiamini hii Qur'ani. Na kwa hivyo wao wanahifadhi kutekeleza Swala kwa ukamilifu na utimilivu.