Skip to content
المَائدة /

Aya 93

5 : 93

Aya 93 of المَائدة (5 : 93). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

المَائدة Aya 120
Sura · المَائدة
Kiswahili · Barawani
5 : 93

لَيۡسَ عَلَى ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ جُنَاحٞ فِيمَا طَعِمُوٓاْ إِذَا مَا ٱتَّقَواْ وَّءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ ثُمَّ ٱتَّقَواْ وَّءَامَنُواْ ثُمَّ ٱتَّقَواْ وَّأَحۡسَنُواْۚ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Si dhambi juu ya walio amini na wakatenda mema kwa walivyo vila (zamani) maadamu wakichamngu na wakiamini na wakitenda mema, kisha wakachamngu, na wakaamini, kisha wakachamngu na wakafanya mazuri. Na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao mazuri.

Explanation & meanings · 1
  1. Walio mkubali Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakatenda mema, hawana dhambi kwa vyakula vya halali na vizuri wanavyo kula, wala vya haramu walivyo wahi kula zamani kabla hawajajua kuwa ni haramu, ikiwa wanamkhofu Mwenyezi Mungu na wakajitenga navyo vyakula hivyo baada ya kujua kuwa vinakatazwa. Kisha ikawa wao wakaendelea kumkhofu Mwenyezi Mungu na kuzikubali sharia zake, na kisha wakadumu katika khofu yao ya kumwogopa Mwenyezi Mungu katika kila hali, na wakawa wanafanya a'mali zao kwa usafi wa niya, na kwa njia ya ukamilifu. Kwani hakika Mwenyezi Mungu huwalipa wenye ikhlasi katika vitendo vyao kwa kadri ya ikhlasi yao na a'mali yao.