Skip to content
Al-Ma'idah /

Aya 92

5 : 92

Aya 92 of Al-Ma'idah (5 : 92). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

Al-Ma'idah Aya 120
Sura · Al-Ma'idah
Kiswahili · Barawani
5 : 92

وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُواْ ٱلرَّسُولَ وَٱحۡذَرُواْۚ فَإِن تَوَلَّيۡتُمۡ فَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ

Na mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume, na tahadharini. Na ikiwa mtageuka basi jueni ya kuwa juu ya Mtume wetu ni kufikisha ujumbe tu ulio wazi.

Explanation & meanings · 1
  1. Na fuateni amri ya Mwenyezi Mungu na amri ya Mtume wake kwa yale anayo kuleteeni kutoka kwa Mola wake Mlezi. Na yaepukeni mbali yatakayo kuleteeni adhabu mnapo kwenda kinyume. Mkitofuata anayo kuamrisheni Mwenyezi Mungu kuweni na yakini kuwa Yeye atakupeni adabu. Wala nyinyi hamna udhuru wowote baada ya kuwa Mtume amekwisha wabainishieni adabu ya kupewa wakhalifu. Na hakika haimpasi Mtume wetu ila kukujuvyeni hukumu zetu tu, na kukubainishieni kwa ukamilifu wa uwazi.