Skip to content
Al-Ma'idah /

Aya 114

5 : 114

Aya 114 of Al-Ma'idah (5 : 114). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

Al-Ma'idah Aya 120
Sura · Al-Ma'idah
Kiswahili · Barawani
5 : 114

قَالَ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَ ٱللَّهُمَّ رَبَّنَآ أَنزِلۡ عَلَيۡنَا مَآئِدَةٗ مِّنَ ٱلسَّمَآءِ تَكُونُ لَنَا عِيدٗا لِّأَوَّلِنَا وَءَاخِرِنَا وَءَايَةٗ مِّنكَۖ وَٱرۡزُقۡنَا وَأَنتَ خَيۡرُ ٱلرَّٰزِقِينَ

Akasema Isa bin Maryamu: Ewe Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wetu! Tuteremshia chakula kutoka mbinguni ili kiwe Sikukuu kwa ajili ya wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu, na kiwe ni Ishara itokayo kwako. Basi turuzuku, kwani Wewe ndiye mbora wa wanao ruzuku.

Explanation & meanings · 1
  1. Isa akawaitikia, na akasema: Ewe Mola wetu Mlezi, uliye miliki mambo yetu yote! Tuteremshie chakula kutoka mbinguni, kiwe ni siku-kuu kwetu kitapo teremka kwa walio amini miongoni mwetu, kwa walio tangulia na walio taakhari, na kiwe ni muujiza wa kutilia nguvu wito wako, na uturuzuku riziki njema, na Wewe ndiye Mbora wa kuruzuku.