Skip to content
النِّسَاء /

Aya 124

4 : 124

Aya 124 of النِّسَاء (4 : 124). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

النِّسَاء Aya 176
Sura · النِّسَاء
Kiswahili · Barawani
4 : 124

وَمَن يَعۡمَلۡ مِنَ ٱلصَّٰلِحَٰتِ مِن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَأُوْلَٰٓئِكَ يَدۡخُلُونَ ٱلۡجَنَّةَ وَلَا يُظۡلَمُونَ نَقِيرٗا

Na anaye fanya mema, akiwa mwanamume au mwanamke, naye ni Muumini - basi hao wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa hata kadiri ya tundu ya kokwa ya tende.

Explanation & meanings · 1
  1. Watendao mema, kwa kadiri ya uwezo wao nao wanamuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wataingia kwenye Pepo ya neema, wala hawatapunguziwa hata chembe. Na hapana khitilafu baina ya malipo ya mwanamume na ya mwanamke, kwani mwanamke naye ana waajibu wake, malipo ya vitendo vyema, na adhabu kwa vitendo vibaya.