Skip to content
An-Nisa /

Aya 123

4 : 123

Aya 123 of An-Nisa (4 : 123). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

An-Nisa Aya 176
Sura · An-Nisa
Kiswahili · Barawani
4 : 123

لَّيۡسَ بِأَمَانِيِّكُمۡ وَلَآ أَمَانِيِّ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِۗ مَن يَعۡمَلۡ سُوٓءٗا يُجۡزَ بِهِۦ وَلَا يَجِدۡ لَهُۥ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلِيّٗا وَلَا نَصِيرٗا

Si kwa matamanio yenu, wala matamanio ya Watu wa Kitabu! Anaye fanya ubaya atalipwa kwalo, wala hatajipatia mlinzi wala wa kumnusuru, isipo kuwa Mwenyezi Mungu.

Explanation & meanings · 1
  1. Malipo siyo ayatamaniyo mtu na kuyaota bila ya vitendo vyema vizaavyo matunda. Malipo siyo myatamaniyo nyinyi, Waislamu. Wala siyo wayatamaniayo na kuyaota Ahlu-l-Kitabi, Watu wa Biblia, Mayahudi na Wakristo. Bali malipo na kuepukana na adhabu ni kwa Imani na Vitendo Vyema. Atendaye maovu atalipwa kwa vitendo vyake. Wala hampati mlinzi wala wa kumnusuru ila Mwenyezi Mungu.