Atakayekula kitunguusaumu, au kitunguu maji, basi na ajitenge nasi, au ajitenge na msikiti wetu, na akae nyumbani kwake
Imepokelewa kutoka kwa Jabiri -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Atakayekula kitunguusaumu, au kitunguu maji, basi na ajitenge nasi, au ajitenge na msikiti wetu, na akae nyumbani kwake", Nakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliletewa chungu kikiwa na mbogamboga, akakuta zinaharufu, akauliza akaelezwa kilichomo katika mboga hizo, akasema: Wapewe baadhi ya Maswahaba zake aliokuwa nao, alipoiona hakupendezwa nayo, akasema: "Kula kwani mimi ninanong'ona na yule usiyenong'ona naye". Na kwa Muslim kutoka kwa Jabiri bin Abdillah, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: “Mwenye kula katika mboga hii, kitunguu saumu." – na mara nyingine alisema: "Mwenye kula kitunguu maji, na kitunguu saumu – asiukaribie msikiti wetu; Kwani hakika Malaika wanaudhika kwa yale ambayo wanadamu wanaudhika nayo.”
«مَنْ أَكَلَ ثُومًا أَوْ بَصَلًا، فَلْيَعْتَزِلْنَا -أَوْ قَالَ: فَلْيَعْتَزِلْ- مَسْجِدَنَا، وَلْيَقْعُدْ فِي بَيْتِهِ»، وَأَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أُتِيَ بِقِدْرٍ فِيهِ خَضِرَاتٌ مِنْ بُقُولٍ، فَوَجَدَ لَهَا رِيحًا، فَسَأَلَ فَأُخْبِرَ بِمَا فِيهَا مِنَ البُقُولِ، فَقَالَ قَرِّبُوهَا إِلَى بَعْضِ أَصْحَابِهِ كَانَ مَعَهُ، فَلَمَّا رَآهُ كَرِهَ أَكْلَهَا، قَالَ: «كُلْ فَإِنِّي أُنَاجِي مَنْ لاَ تُنَاجِي». ولِمُسْلِمٍ عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللهِ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ أَكَلَ مِنْ هَذِهِ الْبَقْلَةِ، الثُّومِ - وقَالَ مَرَّةً: مَنْ أَكَلَ الْبَصَلَ وَالثُّومَ وَالْكُرَّاثَ فَلَا يَقْرَبَنَّ مَسْجِدَنَا، فَإِنَّ الْمَلَائِكَةَ تَتَأَذَّى مِمَّا يَتَأَذَّى مِنْهُ بَنُو آدَمَ».
Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake atakayekula kitunguu saumu au kitunguu maji asije msikitini, ili asiwaudhi ndugu zake katika wale wanaohudhuria swala ya jamaa kwa harufu yake, nalo ni katazo la kiusafi la kutokuja msikitini, na si katazo la kula; kwa sababu ni katika vyakula vya halali, na aliletewa Mtume rehema na amani ziwe juu yake chungu kikiwa na mbogamboga, aliponusa ndani yake harufu au alipoambiwa kilichomo, alikataa kula, na akakisogeza kwa baadhi ya Maswahaba zake akasema: Kula; kwani mimi husema na Malaika kwa wahyi. Na akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Malaika hukereka na harufu mbaya, kama wanavyokereka watu kwa harufu hiyo.
Katazo la kuja msikitini kwa atakayekula kitunguu saumu, au kitunguu maji, au chochote chenye harufu mbaya.
Inaunganishwa na mambo haya, kila chenye harufu mbaya kinachowakera wenye kuswali, kama harufu ya sigara na tumbaku ugoro na mfano wa hivyo.
Sababu ya kukatazwa ni harufu, ikiondoka kwa kupikwa sana au kwa kinginecho; basi chukizo litaondoka.
Chukizo la kula vitu hivi kwa mwenye ulazima wa kuhudhuria swala msikitni; ili jamaa isimpite msikitini, madam hajavila kwa hila ya kukwepa kuhudhuria swala ya jamaa, hapa itakuwa ni haramu.
Mtume rehema na amani ziwe juu yake kukataa kula kitunguu saumu na mfano wake, si kwa ajili ya kuharamisha, bali ni kwa sababu ya mazungumzo yake na Jibril amani iwe juu yake.
Uzuri wa mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kiasi kwamba hukumu anaiambatanisha na sababu yake; ili mkusudiwa atulizane kwa kujua hekima.
Amesema Al-qadhi: Na wanachuoni wametumia kipimo hiki kwa maeneo yote yanayowakusanya watu kwa ajili swala kama viwanja vya Idd na jeneza na mfano wake katika sehemu zinazowakusanya watu kwa ajili ya ibada, na vile vile sehemu wanazokusanyika kwa ajili ya elimu na kumtaja Mwenyezi Mungu na sherehe mbali mbali na mfano wake, isipokuwa masoko na mfano wake hayaingii hapa.
Wamesema wanachuoni: Na katika hadithi hii kuna dalili ya kukataza kula kitunguu saumu na mfano wake wakati wa kuingia msikitini, hata kama pakiwa hakuna mtu ndani yake, kwa sababu ni mahala pa Malaika, na kwa ujumla wa maelekezo ya hadithi.
Swahiih Al Bukhaariy (1/ 170) (855).
Swahiih Muslim (1/ 394) (564).
(1/ 395) (564).
Zaidi (6)
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام.
للبسام (ص204).
تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام.
لابن عثيمين (2/ 260).
تاج العروس من جواهر القاموس.
للزَّبيدي (5/ 332).
Imenukuliwa katika vitabu
8 Vitabu- Fadhila na adabu za Msikiti wa bwana Mtume na hukumu za kuzuru kaburi la Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na kaburi za Maswahaba zake wawili, Mwenyezi Mungu awe radhi naoفضائل وآداب المسجد النبوي، وأحكام زيارة قبر النبي عليه الصلاة والسلام وقبري صاحبيه«Atakayekula kitunguu saumu, au kitunguu maji, basi na ajitenge nasi, au ajitenge na msikiti wetu, na akae nyumbani kwake»[18].
- Imani aliyowafaradhishia Mwenyezi Mungu waja wake kutoka katika yale yaliyokuja katika Qur'ani Tukufu na Sunna za Mtume.“Mwenye kula katika mboga hii, kitunguu saumu." – na mara nyingine alisema: "Mwenye kula kitunguu maji, na kitunguu saumu – asiukaribie msikiti wetu; Kwani hakika Malaika wanaudhika kwa yale ambayo wanadamu wanaudhika nayo.”
Zaidi (6)
- الصلاة التي علمها النبي ﷺ الصحابة رضي الله عنهمالصلاة التي علمها النبي ﷺ الصحابة رضي الله عنهم«مَنْ أَكَلَ مِنْ هَذِهِ الْبَقْلَةِ، الثُّومِ - وقَالَ مَرَّةً: مَنْ أَكَلَ الْبَصَلَ وَالثُّومَ وَالْكُرَّاثَ فَلَا يَقْرَبَنَّ مَسْجِدَنَا، فَإِنَّ الْمَلَائِكَةَ تَتَأَذَّى مِمَّا يَتَأَذَّى مِنْهُ بَنُو آدَمَ»[746].
- الصلاة التي علمها النبي ﷺ الصحابة رضي الله عنهم«مَنْ أَكَلَ مِنْ هَذِهِ الْبَقْلَةِ، الثُّومِ - وقَالَ مَرَّةً: مَنْ أَكَلَ الْبَصَلَ وَالثُّومَ وَالْكُرَّاثَ فَلَا يَقْرَبَنَّ مَسْجِدَنَا، فَإِنَّ الْمَلَائِكَةَ تَتَأَذَّى مِمَّا يَتَأَذَّى مِنْهُ بَنُو آدَمَ»[746].
- رياض الصالحينرياض الصالحين مع فوائد وهدايات - 8«مَنْ أَكَلَ الْبَصَلَ وَالثُّومَ وَالْكُرَّاثَ فَلا يَقْرَبَنَّ مَسْجِدَنَا، فَإنَّ المَلائِكَةَ تَتأذَّىٰ ممَّا يَتَأَذَّىٰ مِنْهُ بَنُو آدَمَ».
- محرمات استهان بها كثير من الناسمن أكل البصل والثوم والكراث فلا يقربن مسجدنا؛ فإن الملائكة تتأذَّى مما يتأذَّى منه بنو آدم
- مشروع منهاج زادكزادك 1 طالب«مَنْ أَكَلَ الْبَصَلَ وَالثُّومَ وَالْكُرَّاثَ فَلاَ يَقْرَبَنَّ مَسْجِدَنَا؛ فَإِنَّ الْمَلاَئِكَةَ تَتَأَذَّى مِمَّا يَتَأَذَّى مِنْهُ بَنُو آدَمَ»
- نبراس طالب (2)نبراس طالب (2) «مَنْ أَكَلَ الْبَصَلَ وَالثُّومَ وَالْكُرَّاثَ فَلاَ يَقْرَبَنَّ مَسْجِدَنَا؛ فَإِنَّ الْمَلاَئِكَةَ تَتَأَذَّى مِمَّا يَتَأَذَّى مِنْهُ بَنُو آدَمَ»