Skip to content

Haki za muislamu juu ya muislamu mwenzake ni tano: Kujibu salamu, na kumtembelea mgonjwa, na kufuata jeneza, na kuitika wito, na kumuombea dua mwenye kupiga chafya

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:

"Haki za muislamu juu ya muislamu mwenzake ni tano: Kujibu salamu, na kumtembelea mgonjwa, na kufuata jeneza, na kuitika wito, na kumuombea dua mwenye kupiga chafya".

«حَقُّ الْمُسْلِمِ عَلَى الْمُسْلِمِ خَمْسٌ: رَدُّ السَّلَامِ، وَعِيَادَةُ الْمَرِيضِ، وَاتِّبَاعُ الْجَنَائِزِ، وَإِجَابَةُ الدَّعْوَةِ، وَتَشْمِيتُ الْعَاطِسِ».

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Ufafanuzi

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baadhi ya haki za muislamu juu ya ndugu yake muislamu, Haki ya kwanza katika hizi ni kujibu salamu kwa atakayekutolea salamu. Haki ya pili: Kumtembelea mgonjwa na kumzuru. Haki ya tatu: Kulifuata jeneza kutoka nyumbani kwake mpaka mahali pa kuswalia mpaka makaburini mpaka kuzika. Haki ya nne: Kuitika wito anapomuita kuja katika walima wa harusi na mengineyo. Haki ya tano: Kumuombea dua mwenye kupiga chafya, nako ni kumwambia -Yarhamukallaah- (Akuhurumie Mwenyezi Mungu) atakapomhimidi Allah kwa kusema (Al-hamdulillah): kisha mpiga chafya amjibu: -Yahdiikumullaahu wayuslih baalakum- (Akuongozeni Allah na akutengenezeeni mambo yenu).

Maana ya Maneno

...:

Katika Faida za Hadithi

Utukufu wa Uislamu katika kuzitilia mkazo haki baina ya waislamu na kuupa nguvu udugu na mapenzi kati yao.

Rejea

Swahiih Al Bukhaariy (2/ 71) (1240).

Swahiih Muslim (4/ 1704) (2162).

Zaidi (10)

كنوز رياض الصالحين.

لمجموعة من الباحثين (4/ 512).

بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين.

لسليم الهلالي (1/ 327).

نزهة المتقين شرح رياض الصالحين.

مجموعة من الباحثين (1/ 253).

شرح رياض الصالحين.

لابن عثيمين (2/ 591).

بهجة قلوب الأبرار.

لابن سعدي (ص81).