Skip to content

Mtu huwa katika mwenendo wa rafiki yake wa karibu, basi na aangalie mmoja wenu ni nani anayemfanya kuwa rafiki yake

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- Amesema:

"Mtu huwa katika mwenendo wa rafiki yake wa karibu, basi na aangalie mmoja wenu ni nani anayemfanya kuwa rafiki yake"

«الرَّجُلُ عَلَى دِينِ خَلِيلِهِ، فَلْيَنْظُر أَحَدُكُم مَنْ يُخَالِل».

Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ahmad
Ni nzuri (Hasan)
Ufafanuzi

Alibainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mtu hufanana na rafiki na jamaa yake wa dhati katika nyenendo na tabia zake, na urafiki huathiri maadili, tabia na matendo, na kwa ajili hiyo alielekeza vyema katika uchaguzi wa rafiki. Kwa sababu atamuongoza rafiki yake katika imani na uongofu na kheri, na atakuwa ni msaada kwa rafiki yake.

Katika Faida za Hadithi

Amri ya kusuhubiana na wema na kuwachambua, na katazo la kusuhubiana na watu wabaya.

Ametajwa rafiki badala ya ndugu; Kwa sababu wewe ndiye unayemchagua rafiki, lakini ndugu na jamaa, huna chaguo.

Kumchukua mtu kuwa rafiki lazima kuanze na kutafakari.

Mtu huiimarisha dini yake kwa kusuhubiana na waumini na huidhoofisha kusuhubiana na watu waovu.

Rejea

Sunanu Abii Daud (7/ 204) (4833).

Sunanu Tirmidhiy (4/ 187) (2378).

Musnad wa Ahmad (13/ 398) (8028).

Zaidi (10)

بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين.

لسليم الهلالي (1/ 433).

تحفة الأحوذي بشرح جامع الترمذي.

للمباركفوري (7/ 51).

تطريز رياض الصالحين.

لفيصل آل مبارك (ص250).

كنوز رياض الصالحين.

لمجموعة من الباحثين (6/ 166).

نزهة المتقين شرح رياض الصالحين.

لمجموعة من الباحثين (1/ 341).