Skip to content
الأنعَام /

Aya 78

6 : 78
الأنعَام Aya 165
Sura · الأنعَام
Kiswahili · Barawani
6 : 78

فَلَمَّا رَءَا ٱلشَّمۡسَ بَازِغَةٗ قَالَ هَٰذَا رَبِّي هَٰذَآ أَكۡبَرُۖ فَلَمَّآ أَفَلَتۡ قَالَ يَٰقَوۡمِ إِنِّي بَرِيٓءٞ مِّمَّا تُشۡرِكُونَ

Na alipo liona jua linachomoza akasema: Huyu ndiye Mola Mlezi wangu. Huyu mkubwa kuliko wote. Lilipo tua, alisema: Enyi watu wangu! Mimi simo katika hayo mnayo fanyia ushirikina.

Explanation & meanings · 1
  1. Tena baada ya hayo, akaliona jua linachomoza. Akasema: Huyu ndiye Mola Mlezi wangu, kwani huyu ni mkubwa kuliko nyota zinavyo onekana. Lilipo kuchwa, likapotea, akasema: Enyi watu wangu! Mimi simo katika kumshirikisha kwenu Mwenyezi Mungu na masanamu kwa kuyaabudu.