Skip to content
الأنعَام /

Aya 79

6 : 79

Aya 79 of الأنعَام (6 : 79). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأنعَام Aya 165
Sura · الأنعَام
Kiswahili · Barawani
6 : 79

إِنِّي وَجَّهۡتُ وَجۡهِيَ لِلَّذِي فَطَرَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ حَنِيفٗاۖ وَمَآ أَنَا۠ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Hakika mimi nimeuelekeza uso wangu sawa sawa kwa aliye ziumba mbingu na ardhi, wala mimi si miongoni mwa washirikina.

Explanation & meanings · 1
  1. Alipo kwisha ona udhaifu wa viumbe alimuelekea aliye viumba, akisema: Mimi nimeyaelekeza makusudio yangu kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu pekee, ambaye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi. Nimejitenga na kila njia isipo kuwa Njia yake Yeye tu. Wala mimi, baada ya nilivyo kwisha ona dalili za Tawhidi (Umoja wa Allah), si katika wanao ridhia kuwa miongoni mwa washirikina kama wao.