Skip to content
الأنعَام /

Aya 77

6 : 77
الأنعَام Aya 165
Sura · الأنعَام
Kiswahili · Barawani
6 : 77

فَلَمَّا رَءَا ٱلۡقَمَرَ بَازِغٗا قَالَ هَٰذَا رَبِّيۖ فَلَمَّآ أَفَلَ قَالَ لَئِن لَّمۡ يَهۡدِنِي رَبِّي لَأَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلضَّآلِّينَ

Alipo uona mwezi unachomoza alisema: Huyu ndiye Mola Mlezi wangu. Ulipotua akasema: Kama Mola Mlezi wangu hakuniongoa, nitakuwa katika kaumu walio potea.

Explanation & meanings · 1
  1. Alipo uona mwezi umechomoza baada ya hayo, akasema akijiambia mwenyewe: Huyu ndiye Mola wangu Mlezi. Ulipo ondoka mwezi, na kukadhihiri kuvunjika ungu wake, akasema ili kuzielekeza nafsi zao ziombe hidaya: Ninaapa, kama Mola Mlezi wangu hakunihidi kwenye Haki, basi hapana shaka nitakuwa katika watu wanao babaika, (wasio jua mojapo la kulishika).