Skip to content
المَائدة /

Aya 66

5 : 66

Aya 66 of المَائدة (5 : 66). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

المَائدة Aya 120
Sura · المَائدة
Kiswahili · Barawani
5 : 66

وَلَوۡ أَنَّهُمۡ أَقَامُواْ ٱلتَّوۡرَىٰةَ وَٱلۡإِنجِيلَ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيۡهِم مِّن رَّبِّهِمۡ لَأَكَلُواْ مِن فَوۡقِهِمۡ وَمِن تَحۡتِ أَرۡجُلِهِمۚ مِّنۡهُمۡ أُمَّةٞ مُّقۡتَصِدَةٞۖ وَكَثِيرٞ مِّنۡهُمۡ سَآءَ مَا يَعۡمَلُونَ

Na lau kuwa wangeli ishika Taurati na Injili na yote waliyo teremshiwa kutokana na Mola wao Mlezi, basi hapana shaka wangeli kula vya juu yao na vya chini ya miguu yao. Wapo watu miongoni mwao walio sawa, lakini wengi wao wanayo yafanya ni mabaya mno.

Explanation & meanings · 1
  1. Na lau kuwa wao wamezihifadhi Taurati na Injili kama zilivyo teremshwa, na wakazitenda, na wakaamini yote waliyo teremshiwa kutokana na Mola wao Mlezi, nayo ni Qur'ani, Mwenyezi Mungu angeli wakunjulia riziki ikiwajia kutoka kila upande. Na wao si wote sawa katika upotovu. Miongoni mwao, wapo jamaa walio waadilifu, wana akili zao timamu. Hao ndio wale walio muamini Muhammad na wakaiamini Qur'ani. Lakini wengi wao wanatenda vitendo viovu, na wanasema mabaya, na wanajitenga na haki.