43 : 77
وَنَادَوۡاْ يَٰمَٰلِكُ لِيَقۡضِ عَلَيۡنَا رَبُّكَۖ قَالَ إِنَّكُم مَّٰكِثُونَ
Nao watapiga kelele waseme: Ewe Malik! Na atufishe Mola wako Mlezi! Naye aseme: Hakika nyinyi mtakaa humo humo!
Explanation & meanings · 1
- Na wakosefu, watapo kwisha kata tamaa ya kupunguziwa adhabu kali, watamwita Malik, huyo ni askari wa Motoni wakimwambia: Mwombe Mola wako Mlezi atufishe tupumzike na adhabu ya Jahannamu. Na Malik awambie: Nyinyi mtakaa humu humu katika adhabu milele!