Skip to content
An-Nisa /

Aya 79

4 : 79

Aya 79 of An-Nisa (4 : 79). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

An-Nisa Aya 176
Sura · An-Nisa
Kiswahili · Barawani
4 : 79

مَّآ أَصَابَكَ مِنۡ حَسَنَةٖ فَمِنَ ٱللَّهِۖ وَمَآ أَصَابَكَ مِن سَيِّئَةٖ فَمِن نَّفۡسِكَۚ وَأَرۡسَلۡنَٰكَ لِلنَّاسِ رَسُولٗاۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدٗا

Jema lilio kufikia limetokana na Mwenyezi Mungu. Na ovu lilio kusibu linatokana na nafsi yako. Nasi tumekutuma kwa watu uwe ni Mtume. Na Mwenyezi Mungu ni shahidi wa kutosha.

Explanation & meanings · 1
  1. Ewe Nabii! Kufanikiwa, na neema, na afya, na salama unayo ipata inatokana na fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yako. Yeye anafanya haya kukufadhili kukufanyia hisani. Na inapo kusibu shida, na mashaka, na udhiya, na ya karaha, basi yanatokana na nafsi yako mwenyewe kwa sababu ya upungufu fulani au makosa uliyo yatenda. Haya anaambiwa Mtume s.a.w. ni kama mfano wa wanaadamu wote ijapo kuwa halikutokea kwake la uovu. Kwani Mtume anaambiwa: Tumekutuma kuwa Mtume kutoka kwetu kwa watu wote. Na Mwenyezi Mungu ni shahidi wa kufikisha kwako huo ujumbe na juu ya kuitikia kwao hao watu. Na Yeye ni Mjuzi wa kutosha.