Skip to content
النِّسَاء /

Aya 69

4 : 69

Aya 69 of النِّسَاء (4 : 69). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

النِّسَاء Aya 176
Sura · النِّسَاء
Kiswahili · Barawani
4 : 69

وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَٱلرَّسُولَ فَأُوْلَٰٓئِكَ مَعَ ٱلَّذِينَ أَنۡعَمَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِم مِّنَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ وَٱلصِّدِّيقِينَ وَٱلشُّهَدَآءِ وَٱلصَّٰلِحِينَۚ وَحَسُنَ أُوْلَٰٓئِكَ رَفِيقٗا

Na wenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume, hao wa pamoja na wale alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, na Masiddiqi, na Mashahidi, na Watu wema. Na uzuri ulioje kuwa pamoja na watu hao!

Explanation & meanings · 1
  1. Na mwenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume kwa kuzifuata kwa unyenyekevu amri zao na kuridhia hukumu yao, basi huyo yu pamoja na alio waneemesha Mwenyezi Mungu kwa uwongofu na kuwawezesha duniani na Akhera. Na watu hao ni Manabii wake, na wafuasi wao walio wasadiki na kuwakubali na wakafuata nyendo zao, na Mashahidi walio kufa katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na watu wema watendao mema kwa siri na dhaahiri. Na hapana la kushinda uzuri kuliko kuwa pamoja na watu hawa - haingii mashakani mwenye kukaa nao, wala hayachoshi mazungumzo yao.