Skip to content
الزُّمَر /

Aya 42

39 : 42

Aya 42 of الزُّمَر (39 : 42). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الزُّمَر Aya 75
Sura · الزُّمَر
Kiswahili · Barawani
39 : 42

ٱللَّهُ يَتَوَفَّى ٱلۡأَنفُسَ حِينَ مَوۡتِهَا وَٱلَّتِي لَمۡ تَمُتۡ فِي مَنَامِهَاۖ فَيُمۡسِكُ ٱلَّتِي قَضَىٰ عَلَيۡهَا ٱلۡمَوۡتَ وَيُرۡسِلُ ٱلۡأُخۡرَىٰٓ إِلَىٰٓ أَجَلٖ مُّسَمًّىۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَتَفَكَّرُونَ

MWENYEZI MUNGU huzipokea roho zinapo kufa. Na zile zisio kufa wakati wa kulala kwake, huzishika zilizo hukumiwa kufa, na huzirudisha nyengine mpaka ufike wakati uliowekwa. Hakika katika hayo bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri.

Explanation & meanings · 1
  1. Mwenyezi Mungu huzitakabadhi roho zinapo kufa. Na huzipokea roho zisio kufa zinapo lala. Basi huzizuia zilizo kwisha hukumiwa kufa, zisirudi kwenye miili yao, na huzirudisha nyenginezo ambazo hazijafikilia bado ajali yao, wakati wa kuamka, mpaka itakapo fika ajali yao ilio wekewa. Hakika katika hayo bila ya shaka zipo Ishara wazi kwa watu wanao zingatia.