Skip to content
الزُّمَر /

Aya 41

39 : 41

Aya 41 of الزُّمَر (39 : 41). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الزُّمَر Aya 75
Sura · الزُّمَر
Kiswahili · Barawani
39 : 41

إِنَّآ أَنزَلۡنَا عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ لِلنَّاسِ بِٱلۡحَقِّۖ فَمَنِ ٱهۡتَدَىٰ فَلِنَفۡسِهِۦۖ وَمَن ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ عَلَيۡهَاۖ وَمَآ أَنتَ عَلَيۡهِم بِوَكِيلٍ

Hakika Sisi tumekuteremshia Kitabu kwa ajili ya watu wote kwa Haki. Basi mwenye kuongoka ni kwa nafsi yake, na mwenye kupotoka bila ya shaka amepotoka kwa khasara yake. Na wewe si mlinzi juu yao.

Explanation & meanings · 1
  1. Ewe Nabii! Hakika Sisi tumekuteremshia Qur'ani Tukufu hii kwa watu wote, nayo imekusanya Haki iliyo thibiti. Basi mwenye kuongoka kwa sababu yake basi manufaa hayo ni kwa nafsi yake, na mwenye kuipotea njia yake basi balaa ya upotofu wake itamrejea mwenyewe. Wala wewe, Muhammad, si mwenye kuwakilishwa uwongofu wao. Jukumu lako ni kufikisha ujumbe, nao umeufikisha.