Skip to content
الزُّمَر /

Aya 37

39 : 37
الزُّمَر Aya 75
Sura · الزُّمَر
Kiswahili · Barawani
39 : 37

وَمَن يَهۡدِ ٱللَّهُ فَمَا لَهُۥ مِن مُّضِلٍّۗ أَلَيۡسَ ٱللَّهُ بِعَزِيزٖ ذِي ٱنتِقَامٖ

Na ambaye Mwenyezi Mungu anamwongoa hana wa kumpotoa. Je! Mwenyezi Mungu si Mwenye nguvu anaye weza kulipiza?

Explanation & meanings · 1
  1. Na mwenye kuongozwa na Mwenyezi Mungu kuendea Haki, na akamwezesha kuifikia, kwa kujua kwake kuwa huyo amekhiari uwongofu kuliko upotovu, basi hatokuwapo wa kumpotoa akaiacha Njia ya Uwongofu. Kwani Mwenyezi Mungu si ndio Yeye ambaye hashindiki kwa kila upande, ambaye ni Mwenye kulipiza kwa ukali? Na kwa hivyo huwalinda vipenzi vyake na maadui wake?