Skip to content
البَقَرَة /

Aya 279

2 : 279

Aya 279 of البَقَرَة (2 : 279). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

البَقَرَة Aya 286
Sura · البَقَرَة
Kiswahili · Barawani
2 : 279

فَإِن لَّمۡ تَفۡعَلُواْ فَأۡذَنُواْ بِحَرۡبٖ مِّنَ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦۖ وَإِن تُبۡتُمۡ فَلَكُمۡ رُءُوسُ أَمۡوَٰلِكُمۡ لَا تَظۡلِمُونَ وَلَا تُظۡلَمُونَ

Basi mkitofanya jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilmali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe.

Explanation & meanings · 1
  1. Ikiwa hamfanyi aliyo kuamrisheni Mwenyezi Mungu kuacha riba basi kuweni na yakini kuwa nyinyi mko vitani na Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa sababu ya inadi yenu kuipinga amri ya Mwenyezi Mungu. Ikiwa mnataka toba ya kukubaliwa basi haki yenu ni kuchukua ile rasilmali yenu tu. Msichukue kitu zaidi, kidogo au kingi, bila ya kujali sababu ya hilo deni na vipi lilivyo tumiwa. Kwani hiyo ziada mnayo ichukua ni kumdhulumu mtu, kama vile kuacha sehemu ya rasilmali yenu ni dhulma juu yenu.