Skip to content
البَقَرَة /

Aya 271

2 : 271

Aya 271 of البَقَرَة (2 : 271). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

البَقَرَة Aya 286
Sura · البَقَرَة
Kiswahili · Barawani
2 : 271

إِن تُبۡدُواْ ٱلصَّدَقَٰتِ فَنِعِمَّا هِيَۖ وَإِن تُخۡفُوهَا وَتُؤۡتُوهَا ٱلۡفُقَرَآءَ فَهُوَ خَيۡرٞ لَّكُمۡۚ وَيُكَفِّرُ عَنكُم مِّن سَيِّـَٔاتِكُمۡۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ

Mkizidhihirisha sadaka ni vizuri; na mkizificha mkawapa mafakiri kwa siri basi hivyo ni kheri kwenu, na yatakuondoleeni baadhi ya maovu yenu. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.

Explanation & meanings · 1
  1. Na ikiwa mtazidhihirisha sadaka zenu, bila ya makusudio ya kutaka kujionyesha kwa watu, ni vizuri kwenu, inapendeza, na kwa Mola wenu Mlezi inasifika. Na pindi mkiwapa mafakiri kwa siri ili msiwatie haya, na kwa kuogopa riya (kujionyesha), basi nayo ni kheri kwenu. Na Mwenyezi Mungu atakusameheni dhambi zenu kwa sababu ya usafi wa niya zenu katika kutoa sadaka zenu. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayo yaficha na mnayo yadhihirisha, na anazijua niya zenu mnapo dhihirisha na mnapo ficha.