Skip to content
الإسرَاء /

Aya 34

17 : 34

Aya 34 of الإسرَاء (17 : 34). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الإسرَاء Aya 111
Sura · الإسرَاء
Kiswahili · Barawani
17 : 34

وَلَا تَقۡرَبُواْ مَالَ ٱلۡيَتِيمِ إِلَّا بِٱلَّتِي هِيَ أَحۡسَنُ حَتَّىٰ يَبۡلُغَ أَشُدَّهُۥۚ وَأَوۡفُواْ بِٱلۡعَهۡدِۖ إِنَّ ٱلۡعَهۡدَ كَانَ مَسۡـُٔولٗا

Wala msiyakaribie mali ya yatima, isipo kuwa kwa njia iliyo bora, mpaka afike utuuzimani. Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itasailiwa.

Explanation & meanings · 1
  1. Wala msiyatumie mali ya yatima ila kwa njia iliyo bora kabisa, ya kuiamirisha na kuikuza. Na endeleeni hivyo mpaka huyo mtoto afike umri wa utambuzi kuweza kuendesha mambo yake. Na akisha fika hivyo basi mkabidhini mali yake, na timizeni ahadi zote mlizo chukua. Kwani Mwenyezi Mungu atamsaili (atamuliza) aliye vunja ahadi kwa kuvunja kwake, na atamhisabia kwa hayo.