Skip to content
هُود /

Aya 100

11 : 100
هُود Aya 123
Sura · هُود
Kiswahili · Barawani
11 : 100

ذَٰلِكَ مِنۡ أَنۢبَآءِ ٱلۡقُرَىٰ نَقُصُّهُۥ عَلَيۡكَۖ مِنۡهَا قَآئِمٞ وَحَصِيدٞ

Hizi ni katika khabari za miji, tunakusimulia. Mingine ipo bado na mingine imefyekwa.

Explanation & meanings · 1
  1. Hadithi hio, ewe Nabii, ni baadhi ya khabari za miji tuliyo iteketeza. Tunakusimulia wewe upate kuwatolea mawaidha kwa khabari hizo watu wako, na utumaini kuwa Mwenyezi Mungu atakunusuru. Baadhi ya miji hiyo imekuwa kama mimea iliyo simama juu ya mashina yake ili waone yaliyo tokea, na baadhi yao imefutika athari yake kama mazao yaliyo kwisha vunwa.