Skip to content
Hud /

Aya 101

11 : 101

Aya 101 of Hud (11 : 101). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

Hud Aya 123
Sura · Hud
Kiswahili · Barawani
11 : 101

وَمَا ظَلَمۡنَٰهُمۡ وَلَٰكِن ظَلَمُوٓاْ أَنفُسَهُمۡۖ فَمَآ أَغۡنَتۡ عَنۡهُمۡ ءَالِهَتُهُمُ ٱلَّتِي يَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مِن شَيۡءٖ لَّمَّا جَآءَ أَمۡرُ رَبِّكَۖ وَمَا زَادُوهُمۡ غَيۡرَ تَتۡبِيبٖ

Na Sisi hatukuwadhulumu, lakini wao wenyewe wamejidhulumu. Na miungu yao waliyo kuwa wakiiomba badala ya Mwenyezi Mungu haikuwafaa kitu ilipo kuja amri ya Mola wako Mlezi. Na hiyo miungu haikuwazidishia ila maangamizo tu.

Explanation & meanings · 1
  1. Wala Sisi hatukuwadhulumu kwa vile tulivyo wateketeza; lakini wamejidhulumu wenyewe kwa kufuru zao, na kuacha kumuabudu Mwenyezi Mungu, na kuleta uharibifu katika nchi. Kwa hivyo miungu yao waliyo kuwa wakiiabudu badala ya Mwenyezi Mungu haikuweza kuwakinga na hilaki, wala haikuwafaa kitu ilipo kuja amri ya Mola wako Mlezi, ewe Nabii! Na kushikilia kwao kuabudu masanamu hakukuwazidishia ila hilaki na upotovu!