10 : 105
وَأَنۡ أَقِمۡ وَجۡهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفٗا وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ
Na uelekeze uso wako kwenye Dini ya Kweli, wala usiwe katika washirikina.
Explanation & meanings · 1
- Ewe Nabii! Simama sawasawa, umuelekee Mwenyezi Mungu vilivyo. Wala usijitie katika miongoni mwa walio mshirikisha Mwenyezi Mungu. Epukana nao, na uwe mbali nao, wewe na Waumini wanao kufuata.