Hakita simama Kiyama mpaka jua lichomoze kutoka upande wa Magharibi, na likichomoza na wakaliona watu wote wataamini
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
"Hakita simama Kiyama mpaka jua lichomoze kutoka upande wa Magharibi, na likichomoza na wakaliona watu wote wataamini, na wakati huo: ((Mtu haitamfaa imani yake ambaye alikuwa hakuamini kabla, au imani yake haikufanya mambo ya kheri:158)) na kwa hakika kitasimama Kiyama na hali yakuwa watu wawili wametandaza nguo zao kwa ajili ya kuuza na kununua na wala hatoweza kuzikunja kutokana na uharaka wa Kiyama, na kwa hakika kitasimama Kiyama ghafla, na kwa hakika ataondoka mtu na maziwa aliyoyachukua kwenye chuchu za mnyama na wala asiwahi kuyanywa, na kitasimama Kiyama wakati anatengeneza josho la kunyweshea na wala asiwahi kunywesheleza, na kwa hakika kitasimama Kiyama na mmmoja wenu atainua tonge kupeleka mdomoni na wala asiweze kula."
«لاَ تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ مِنْ مَغْرِبِهَا، فَإِذَا طَلَعَتْ فَرَآهَا النَّاسُ آمَنُوا أَجْمَعُونَ، فَذَلِكَ حِينَ: {لاَ يَنْفَعُ نَفْسًا إِيمَانُهَا لَمْ تَكُنْ آمَنَتْ مِنْ قَبْلُ، أَوْ كَسَبَتْ فِي إِيمَانِهَا خَيْرًا} [الأنعام: 158] وَلَتَقُومَنَّ السَّاعَةُ وَقَدْ نَشَرَ الرَّجُلاَنِ ثَوْبَهُمَا بَيْنَهُمَا فَلاَ يَتَبَايَعَانِهِ، وَلاَ يَطْوِيَانِهِ، وَلَتَقُومَنَّ السَّاعَةُ وَقَدِ انْصَرَفَ الرَّجُلُ بِلَبَنِ لِقْحَتِهِ فَلاَ يَطْعَمُهُ، وَلَتَقُومَنَّ السَّاعَةُ وَهُوَ يَلِيطُ حَوْضَهُ فَلاَ يَسْقِي فِيهِ، وَلَتَقُومَنَّ السَّاعَةُ وَقَدْ رَفَعَ أَحَدُكُمْ أُكْلَتَهُ إِلَى فِيهِ فَلاَ يَطْعَمُهَا».
Anatoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa miongoni mwa alama kubwa za Kiyama, ni kuchomoza jua kutoka upande wa Magharibi badala ya upande wa Mashariki, na watu wakiliona wataamini wote, Na wakati huo haitomfaa kafiri imani yake, wala hayatomfaa matendo mema wala kutubia. Kisha akatoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Kiyama kitatokea ghafla; Kitatokea na watu watakuwa kwenye hali walizokuwa nazo na wapo kwenye mambo yao ya kimaisha; Na kitasimama Kiyama hali ya kuwa muuzaji na mnunuzi wamesambaza nguo zao lakini hawataweza kuuziana wala hawataweza kuzikunja. Na kitasimama Kiyama na hali ya kuwa mtu ameshika maziwa aliyoyakamua kutoka kwa Ngamia wake na wala hatoweza kuyanywa. Na kitasimama Kiyama na mtu atakuwa anatengeneza josho la kunyweshezea wanyama na kulisiriba na wala hatowahi kunywesheleza humo. Na kitasimama Kiyama na mtu atakuwa kainua tonge lake ili kulipeleka kinywani mwake ili ale na wala hatoweza kulila tonge hilo.
...:
Uislamu na toba hukubalika kabla jua halijatoka upande wa Magharibi.
Kuhimizwa kujiandaa kwa ajili ya Kiyama kwa kuwa na imani na kutenda yaliyo mema; Kwa sababu Kiyama kitakuja ghafla.
Swahiih Al Bukhaariy (8/ 106) (6506).
Swahiih Muslim (1/ 137) (157).
Zaidi (1)
عمدة القاري شرح صحيح البخاري (23/ 92).
Imenukuliwa katika vitabu
2 Vitabu- Imani aliyowafaradhishia Mwenyezi Mungu waja wake kutoka katika yale yaliyokuja katika Qur'ani Tukufu na Sunna za Mtume."Hakitosimama Kiyama mpaka jua litakapochomozea Magharibi mwake. Litakapochomozea Magharibi mwake, watu wote kwa pamoja wataamini, na siku hiyo ndiyo "kuamini hapo hakutomfaa mtu kitu, ikiwa hakuwa ameamini kabla yake." [Al-An'am: 158]
- Imani aliyowafaradhishia Mwenyezi Mungu waja wake kutoka katika yale yaliyokuja katika Qur'ani Tukufu na Sunna za Mtume."... Na hakika Saa itasimama hali ya kuwa wanaume wawili wanataka kuuziana nguo zao, lakini hawatauziana wala kuzikunja (kabla ya Saa kusimama). Na hakika Saa itasimama hali ya kuwa mtu mmoja ameshaondoka na maziwa ya ngamia wake, lakini w