Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi, hakika Shetani hukimbia kutoka katika nyumba inayosomwa suratul Baqara ndani yake
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi, hakika Shetani hukimbia kutoka katika nyumba inayosomwa suratul Baqara ndani yake".
«لَا تَجْعَلُوا بُيُوتَكُمْ مَقَابِرَ، إِنَّ الشَّيْطَانَ يَنْفِرُ مِنَ الْبَيْتِ الَّذِي تُقْرَأُ فِيهِ سُورَةُ الْبَقَرَةِ».
Anakataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuyatelekeza majumba kwa kutoka swali ndani yake, yakawa kama makaburi yasiyoswaliwa ndani yake. Kisha akaeleza -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Shetani hukimbia nyumba ambayo husomwa suratul Baqara ndani yake.
ينفر: يصد ويعرض إعراضاً بالغاً.
Kumependekezwa kuzidisha ibada na swala za sunna ndani ya majumba.
Haifai kuswali makaburini; kwa sababu ni njia katika njia za shirki na kuwakweza wafu, isipokuwa swala ya jeneza.
Katazo la kuswali makaburini limethibiti kwa Masahaba, na kwa sababu hiyo amekataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nyumba kufanywa mfano wa makaburi hakuswaliwi ndani yake.
Swahiih Muslim (1/ 539) (780).
Zaidi (8)
بهجة الناظرين.
لسليم الهلالي (2/ 240).
شرح رياض الصالحين.
لابن عثيمين (4/ 682).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين.
لمصطفى الخِن وغيره (2/ 757).
مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح.
لعلي القاري (4/ 1460).
Imenukuliwa katika vitabu
4 Vitabu- YALIYO CHAGULIWA KUTOKA KATIKA SOKO LENYE FAIDA KATIKA THAWABU ZA MATENDO MEMA.المنتقى من المتجر الرابح في ثواب العمل الصالح"Msiyafanye Majumba yenu kuwa ni makaburi, hakika shetani hukimbia nyumba ambayo husomwa ndani yake suratul-baqara".
- Hisnu Al-Muslim Kutoka Katika Nyiradi Za Kitabu Na Sunnaحصن المسلم"Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi. Hakika Shetani hukimbia kutoka katika nyumba inayosomwa suratul Baqara ndani yake."[184]