Pokea habari njema ya kupewa Nuru mbili hakupewa Nabii yeyote kabla yako: Ufunguzi wa kitabu (Alfatiha) na Aya za mwisho katika Suratul-baqarah, hautasoma herufi miongoni mwa Sura hizo mbili isipokuwa utapewa (unacho hitaji)
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema:
"Pindi Jibrili alipokuwa amekaa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisikia kishindo kutoka juu yake, akanyanyua kichwa chake, akasema: "Huu ni mlango kutoka Mbinguni umefunguliwa leo haukuwahi kufunguliwa kabisa isipokuwa leo, kisha akateremka kutoka kwenye mlango ule Malaika, akasema: "Huyu ni Malaika ameteremka Ardhini hakupata kuteremka kabisa isipokuwa leo, akawasalimia, kisha akasema: "Pokea habari njema ya kupewa Nuru mbili hakupewa Nabii yeyote kabla yako: Ufunguzi wa kitabu (Alfatiha) na Aya za mwisho katika Suratul-baqarah, hautasoma herufi miongoni mwa Sura hizo mbili isipokuwa utapewa (unacho hitaji)"
«بَيْنَمَا جِبْرِيلُ قَاعِدٌ عِنْدَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سَمِعَ نَقِيضًا مِنْ فَوْقِهِ، فَرَفَعَ رَأْسَهُ، فَقَالَ: هَذَا بَابٌ مِنَ السَّمَاءِ فُتِحَ الْيَوْمَ لَمْ يُفْتَحْ قَطُّ إِلَّا الْيَوْمَ، فَنَزَلَ مِنْهُ مَلَكٌ، فَقَالَ: هَذَا مَلَكٌ نَزَلَ إِلَى الْأَرْضِ لَمْ يَنْزِلْ قَطُّ إِلَّا الْيَوْمَ، فَسَلَّمَ، وَقَالَ: أَبْشِرْ بِنُورَيْنِ أُوتِيتَهُمَا لَمْ يُؤْتَهُمَا نَبِيٌّ قَبْلَكَ: فَاتِحَةُ الْكِتَابِ، وَخَوَاتِيمُ سُورَةِ الْبَقَرَةِ، لَنْ تَقْرَأَ بِحَرْفٍ مِنْهُمَا إِلَّا أُعْطِيتَهُ».
Malaika Jibril amani iwe juu yake alikuwa amekaa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasikia sauti kutoka mbinguni kama sauti ya mlango unapofunguliwa, Jibril akanyanyua kichwa chake na macho yake mbinguni, kisha akaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba mlango huu kutoka mbinguni umefunguliwa leo, na haukuwahi kufunguliwa katu isipokuwa leo, akateremka kutoka humo Malaika kuja Ardhini, hakuwahi kuteremka kabla isipokuwa leo, Malaika akamtolea salamu Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akasema kumwambia: Kuwa na habari njema ya kupata Nuru mbili ulizopewa, ambazo hakuwahi kupewa Nabii yeyote kabla yako; nazo ni: Suratul-Fatiha, na Aya mbili za mwisho wa suratul-Baqara. Kisha Malaika akasema: Hatosoma yeyote harufi moja katika hizo isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa yale yaliyomo ndani yake miongoni mwa heri na dua na maombi.
Fadhila za Suratul-Fatiha na mwisho wa Suratul-Baqara, na himizo la kuzisoma na kuyafanyia kazi mafundisho yake.
Mbingu zina milango ambayo huteremka amri za Mola kupitia hapo, na wala hazifunguliwi isipokuwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Kumebainishwa takrima za Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Mola wake Mlezi, kiasi ambacho amemkirimu kwa mambo ambayo hakuwakirimu Manabii waliokuwa kabla yake, akampatia Nuru hizi mbili.
Miongoni mwa nyenzo za kuwalingania watu kwa Mwenyezi Mungu ni kuwapa habari njema.
Swahiih Muslim (1/ 554) (806).
Zaidi (10)
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين.
لسليم الهلالي (2/ 244).
شرح رياض الصالحين.
لابن عثيمين (4/ 700).
مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح.
لعلي القاري (4/ 1464).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين.
لمجموعة من الباحثين (2/ 760).
كنوز رياض الصالحين.
لمجموعة من الباحثين (13/ 122).
Imenukuliwa katika vitabu
6 Vitabu- YALIYO CHAGULIWA KUTOKA KATIKA SOKO LENYE FAIDA KATIKA THAWABU ZA MATENDO MEMA.المنتقى من المتجر الرابح في ثواب العمل الصالح"Pindi Jibrili alipokuwa amekaa kwa Mtume Sala na amani ziwe juu yake alisikia kishindo kutoka juu yake, akanyanyua kichwa chake, akasema: "Huu ni mlango kutoka Mbinguni umefunguliwa leo hakuwahi kufunguliwa kabisa isipokuwa leo, kisha akat
- Imani aliyowafaradhishia Mwenyezi Mungu waja wake kutoka katika yale yaliyokuja katika Qur'ani Tukufu na Sunna za Mtume.Na imesimuliwa kutoka kwa Ibn Abbas, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wawili, kuwa alisema: Jibril alipokuwa ameketi pamoja na Mtume Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alisikia sauti kutokea juu yake, akainua kichwa chake na akase
- Imani aliyowafaradhishia Mwenyezi Mungu waja wake kutoka katika yale yaliyokuja katika Qur'ani Tukufu na Sunna za Mtume.Imesimuliwa kutoka kwa Ibn Abbas, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, kuwa alisema: Jibril alipokuwa amekaa na Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alisikia sauti kutokea juu yake, akainua kichwa chake na akasema: “H
Zaidi (3)
- الخطب المنبريةموسوعة الخطب المنبرية (القسم الثالث)«أَبْشِرْ بِنُورَيْنِ أُوتِيتَهُمَا لَمْ يُؤْتِهِمَا نَبِيٌّ قَبْلَكَ: فَاتِحَةُ الْكِتَابِ، وَخَوَاتِيمُ سُورَةِ الْبَقَرَةِ لَمْ تَقْرَأْ حَرْفًا مِنْهَا إِلَّا أُوتِيتَهُ»
- مجالس تدارس القرآن للمبتدئين (سورة الفاتحة وقصار المفصّل)1(أبشر بنورين أوتيتهما لم يؤتهما نبي قبلك: فاتحة الكتاب، وخواتيم سورة البقرة)([6]).
- مجموعة زاد التفسير (1)التفسير 1بَيْنَما جِبْرِيلُ عليه السلام قاعِدٌ عِنْدَ النبيِّ صلى الله عليه وسلم سَمِعَ نَقِيضا مِنْ فَوقِهِ فَرَفَعَ رأسَهُ، فقال:«هَذا بابٌ مِنَ السَّماءِ فُتِحَ اليَومَ لَمْ يُفْتَحْ قَطُّ إلا اليَومَ، فَنزَلَ مِنهُ مَلَكٌ، فقال: هَذا مَلَكٌ نَزَ