Skip to content

Yeyote atakayefanya wema katika Uislamu basi hatoadhibiwa kwa yale aliyoyatenda katika zama za ujinga, na yeyote atakaye tenda maovu akiwa katika Uislamu ataadhibiwa kwa makosa yake ya mwanzo na ya mwisho

Imepokelewa hadithi kutoka kwa bin Masoud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-, amesema:

Alisema mtu mmoja: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hivi sisi tutaadhibiwa kwa tuliyoyafanya katika zama za ujinga kabla yakuwa waislamu?Akasema "Yeyote atakayefanya wema katika Uislamu basi hatoadhibiwa kwa yale aliyoyatenda katika zama za ujinga, na yeyote atakaye tenda maovu akiwa katika Uislamu ataadhibiwa kwa makosa yake ya mwanzo na ya mwisho".

قَالَ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اللهِ، أَنُؤَاخَذُ بِمَا عَمِلْنَا فِي الْجَاهِلِيَّةِ؟ قَالَ: «مَنْ أَحْسَنَ فِي الْإِسْلَامِ لَمْ يُؤَاخَذْ بِمَا عَمِلَ فِي الْجَاهِلِيَّةِ، وَمَنْ أَسَاءَ فِي الْإِسْلَامِ أُخِذَ بِالْأَوَّلِ وَالْآخِرِ».

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Ufafanuzi

Anatuwekea wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ubora wa kuingia katika Uislamu, Na kuwa mwenye kusilimu na uislamu wake ukawa mzuri na akawa mtakasifu na mkweli, basi hatoadhibiwa kwa makosa aliyoyafanya kabla ya uislamu, Na atakaye fanya uovu akiwa katika uislamu, yaani kwa kuwa mnafiki au akatoka katika dini yake, basi huyo ataadhibiwa kwa aliyoyafanya akiwa bado hajaingia katika uislamu na ataadhibiwa pia kwa yale aliyoyafanya akiwa katika uislamu.

Maana ya Maneno

...:

Katika Faida za Hadithi

Maswahaba -Radhi za Allah ziwe juu yao- kutilia umuhimu mambo mazito, na hofu yao kwa yale yaliyokuwa kabla ya Uislamu.

Mahimizo ya kudumu kwenye Uislamu.

Ubora na fadhila za kuingia katika uislamu, na kuingia katika uislamu hufuta matendo mabaya yaliyopita.

Mwenye kutoka katika uislamu na mnafiki, atahukumiwa kwa kila kitendo alichokifanya kabla ya kusilimu kwake, na kuhukumiwa kwa dhambi alilofanya kwenye uislamu.

Rejea

Swahiih Al Bukhaariy (9/ 14) (6921).

Swahiih Muslim (1/ 111) (120).

Zaidi (3)

مشارق الأنوار على صحاح الآثار (2/229).

الكواكب الدراري (24/43).

عمدة القاري شرح صحيح البخاري (24/ 76).