Atakapoingia mmoja wenu msikitini basi aseme: Allaahummaf-tah lii abwaaba rahmatika (Ewe Mola wangu, nifungulie milango ya rehema zako), na akitoka aseme: Allaahumma innii as-aluka min fadhlika (Ewe Mola wangu ninakuomba unipe katika fadhila zako)
Kutoka kwa Abuu Humaidi au kutoka kwa Abuu Usaidi Amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Atakapoingia mmoja wenu msikitini basi aseme: Allaahummaf-tah lii abwaaba rahmatika (Ewe Mola wangu, nifungulie milango ya rehema zako), na akitoka aseme: Allaahumma innii as-aluka min fadhlika (Ewe Mola wangu ninakuomba unipe katika fadhila zako)".
«إِذَا دَخَلَ أَحَدُكُمُ الْمَسْجِدَ فَلْيَقُلِ: اللَّهُمَّ افْتَحْ لِي أَبْوَابَ رَحْمَتِكَ، وَإِذَا خَرَجَ فَلْيَقُلِ: اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ فَضْلِكَ».
Ameuelekeza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- umma wake katika dua ambayo husemwa wakati wa kuingia msikitini: "Allaahummaf-tah lii abwaaba rahmatika (Ewe Mola wangu, nifungulie milango ya rehema zako), amuombe Mwenyezi Mungu Mtukufu amuandalie sababu za kupata rehema zake, na akitaka kutoka aseme: Allaahumma innii as-aluka min fadhlika (Ewe Mola wangu ninakuomba unipe katika fadhila zako), amuombe Mwenyezi Mungu Mtukufu ampe katika fadhila zake na ziada ya hisani zake miongoni mwa riziki ya halali.
Sunna ya dua hii wakati wa kuingia msikitini na wakati wa kutoka.
Zimetengwa rehema wakati wa kuingia, na fadhila wakati wa kutoka: Kwani mwenye kuingia hushughulika na yale yanayomkurubisha kwa Allah na katika Pepo yake ikawa ni bora ataje rehema, na anapotoka hutembea katika Ardhi kwa ajili ya kutafuta fadhila za Allah miongoni mwa riziki, ikawa ni bora kwake kutaja fadhila.
Dua hizi husomwa wakati wa kutaka kuingia msikitini, na wakati wa kutaka kutoka.
Swahiih Muslim (1/ 494) (713).
Zaidi (3)
الكاشف عن حقائق السُّنن (3/935).
فيض القدير (1/ 336).
ذخيرة العقبى (9/153).
Imenukuliwa katika vitabu
10 Vitabu- Hisnu Al-Muslim Kutoka Katika Nyiradi Za Kitabu Na Sunnaحصن المسلمAllahumma inni as'aluka min fadhlik
- Fadhila na adabu za Msikiti wa bwana Mtume na hukumu za kuzuru kaburi la Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na kaburi za Maswahaba zake wawili, Mwenyezi Mungu awe radhi naoفضائل وآداب المسجد النبوي، وأحكام زيارة قبر النبي عليه الصلاة والسلام وقبري صاحبيه"Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba unipe katika fadhila zako"[19],
Zaidi (8)
- الذكر والدعاء والعلاج بالرقي من الكتاب والسنة"إذا دخل أحدكم المسجد فليقل: اللهم افتح لي أبواب رحمتك. وإذا خرج فليقل: اللهم إني أسألك من فضلك".
- المختصر في آداب السفر وصفة الحج والعمرة وآداب الزيارة والأدعية الجامعة مع ملحق بالفتاوى والمخالفات2- المختصر في صفة الحج وأحكامه (للحرمين)«اللَّهُمَّ افْتَحْ لِي أَبْوَابَ رَحْمَتِكَ»[2]،
- المختصر في صفة الحج وأحكامهالمختصر في صفة الحج والعمرة«اللَّهُمَّ افْتَحْ لِي أَبْوَابَ رَحْمَتِكَ»[2]،
- رسالة في الأذكار1«إِذَا دَخَلَ أَحَدُكُمُ المَسْجِدَ فَلْيَقُلِ: اللَّهُمَّ افْتَحْ لِي أَبْوَابَ رَحْمَتِكَ، وَإِذَا خَرَجَ فَلْيَقُلِ: اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ فَضْلِكَ».
- ما لا يسع أطفال المسلمين جهله«اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ فَضْلِكَ»[150].
- ما لا يسع أطفال المسلمين جهلهج: «اللَّهُمَّ افْتَحْ لِي أَبْوَابَ رَحْمَتِكَ»[221].
- ما لا يسع أطفال المسلمين جهلهج: «اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ فَضْلِكَ»[222].
- مجموعة زاد التربية الإسلامية (3)، والسيرة النبوية (3)التربية الإٍسلامية -3- «اللهم إني أسألك من فضلك»