Hakika muumini hufikia kwa sababu ya tabia zake njema daraja ya mfungaji mwenye kusimama usiku
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Hakika muumini hufikia kwa sababu ya tabia zake njema daraja ya mfungaji mwenye kusimama usiku".
«إنَّ المُؤْمِنَ ليُدرِكُ بِحُسْنِ خُلُقِهِ دَرَجَةَ الصَّائِمِ القَائِمِ».
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa tabia njema humfikisha mwenye tabia hiyo nafasi ya mwenye kufunga mchana daima na kusimama usiku, na tabia njema inakusanywa na: Kutenda wema, na kauli nzuri, na uso mkunjufu, na kuacha maudhi na kuyavumilia kutoka kwa watu.
....:
Uislamu umetilia umuhimu mkubwa kurekebisha tabia na ukamilifu wake.
Ubora wa tabia njema, mpaka mja humfikisha daraja ya mfungaji asiyefungua na mwenye kusimama usiku asiyechoka.
Kufunga mchana na kusimama usiku ni amali mbili kubwa, kuna uzito mkubwa sana kwa nafsi, lakini daraja yake ameifikia mwenye tabia njema kwa kupambana na nafsi yake ili kuwa na muamala mzuri na watu.
Sunanu Abii Daud (7/ 176) (4798).
Musnad wa Ahmad (40/ 414) (24355).
Zaidi (6)
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين.
لسليم الهلالي (1/ 675).
تطرز رياض الصالحين.
لفيصل آل مبارك (ص411).
مشكاة المصابيح.
لمحمد العمري (3/ 1409).
Imenukuliwa katika vitabu
6 VitabuZaidi (6)
- الحقيقة المُبْهِرَة في العلاقة بين الإسلام والإنسان(إن المؤمن ليدرك بحُسْن خُلُقه درجة الصائم القائم)[132].
- رياض الصالحينرياض الصالحين مع فوائد وهدايات - 3«إنَّ المُؤْمِنَ لَيُدْرِكُ بِحُسْنِ خُلُقِهِ دَرَجَةَ الصَّائِمِ القَائِمِ».
- مشروع منهاج زادكزادك 2 طالب نهائي«إِنَّ الْمُؤْمِنَ لَيُدْرِكُ بِحُسْنِ خُلُقِهِ دَرَجَةَ الصَّائِمِ الْقَائِمِ»
- نبراس طالب (2)نبراس طالب (2) «إِنَّ الْمُؤْمِنَ لَيُدْرِكُ بِحُسْنِ خُلُقِهِ دَرَجَةَ الصَّائِمِ الْقَائِمِ»
- وثيقة منهج نبراس لمدارس نهاية الأسبوع1"إن المؤمن ليدرك بحسن خلقه درجة الصائم القائم"
- وثيقة منهج نبراس لمدارس نهاية الأسبوع1"إن المؤمن ليدرك بحسن خلقه درجة الصائم القائم"