Skip to content
Al-Anfal /

Aya 67

8 : 67

Aya 67 of Al-Anfal (8 : 67). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

Al-Anfal Aya 75
Sura · Al-Anfal
Kiswahili · Barawani
8 : 67

مَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَكُونَ لَهُۥٓ أَسۡرَىٰ حَتَّىٰ يُثۡخِنَ فِي ٱلۡأَرۡضِۚ تُرِيدُونَ عَرَضَ ٱلدُّنۡيَا وَٱللَّهُ يُرِيدُ ٱلۡأٓخِرَةَۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٞ

Haimfalii Nabii yeyote kuwa na mateka mpaka awe ameshinda baraabara katika nchi. Mnataka vitu vya dunia, na Mwenyezi Mungu anataka Akhera. Na Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mwenye nguvu Mwenye hikima.

Explanation & meanings · 1
  1. Haimfalii Nabii yeyote kukamata mateka, au kuchukua fidia, au kutoa bure msamaha, mpaka ashinde, na maadui waone wameshindwa, na wawe wamepata pigo kubwa hata kuwa hawawezi tena kupigana katika nchi. Lakini, nyinyi jamaa wa Kiislamu, mmefanya haraka katika Vita vya Badri kukamata mateka kabla hamjatamakani mkawa imara katika nchi. Mnatafuta manufaa ya dunia, na Mwenyezi Mungu anataka Akhera, kwa kutukuzwa Neno la Haki, na lisikushughulisheni la dunia. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda. Hukupangieni mambo yenu kwa mujibu wa faida yenu.