76 : 22
إِنَّ هَٰذَا كَانَ لَكُمۡ جَزَآءٗ وَكَانَ سَعۡيُكُم مَّشۡكُورًا
Hakika haya ni malipo yenu; na juhudi zenu zimekubaliwa.
Explanation & meanings · 1
- Hakika neema hizi ameziandaa kwa kukulipeni kwa vitendo vyenu. Na hizo juhudi zenu duniani ni zenye kusifika kwa Mwenyezi Mungu, na zinampendeza, na zimekubaliwa.