Skip to content
الأنعَام /

Aya 80

6 : 80

Aya 80 of الأنعَام (6 : 80). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأنعَام Aya 165
Sura · الأنعَام
Kiswahili · Barawani
6 : 80

وَحَآجَّهُۥ قَوۡمُهُۥۚ قَالَ أَتُحَٰٓجُّوٓنِّي فِي ٱللَّهِ وَقَدۡ هَدَىٰنِۚ وَلَآ أَخَافُ مَا تُشۡرِكُونَ بِهِۦٓ إِلَّآ أَن يَشَآءَ رَبِّي شَيۡـٔٗاۚ وَسِعَ رَبِّي كُلَّ شَيۡءٍ عِلۡمًاۚ أَفَلَا تَتَذَكَّرُونَ

Na watu wake wakamhoji. Akasema: Je, mnanihoji juu ya Mwenyezi Mungu, na hali Yeye ameniongoa? Wala siogopi hao mnao washirikisha naye, ila Mola wangu Mlezi akipenda kitu. Mola wangu Mlezi amekusanya ilimu ya kila kitu. Basi je, hamkumbuki?

Explanation & meanings · 1
  1. Na juu ya hivyo, watu wake walijadiliana naye katika Umoja wa Mwenyezi Mungu, na wakamtisha kuwa atapata ghadhabu ya miungu yao. Basi yeye akawaambia: Haikufaliini nyinyi kuzozana nami katika Umoja wa Mwenyezi Mungu, naye amekwisha nihidi kufikia Haki. Wala siogopi ghadhabu ya miungu yenu mnayo ifanya ni washirika wa Mwenyezi Mungu. Lakini Mola wangu Mlezi akipenda madhara yatatokea, kwa kuwa Yeye pekee ndiye Muweza. Naye Mola wangu Mlezi amekusanya ilimu ya vitu vyote, na hao miungu yenu haina chochote inacho jua! Je, mmeghafilika na yote hayo, na hamtambui kuwa mjinga aliye emewa hastahiki kuabudiwa?