Skip to content
Al-An'am /

Aya 158

6 : 158

Aya 158 of Al-An'am (6 : 158). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

Al-An'am Aya 165
Sura · Al-An'am
Kiswahili · Barawani
6 : 158

هَلۡ يَنظُرُونَ إِلَّآ أَن تَأۡتِيَهُمُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ أَوۡ يَأۡتِيَ رَبُّكَ أَوۡ يَأۡتِيَ بَعۡضُ ءَايَٰتِ رَبِّكَۗ يَوۡمَ يَأۡتِي بَعۡضُ ءَايَٰتِ رَبِّكَ لَا يَنفَعُ نَفۡسًا إِيمَٰنُهَا لَمۡ تَكُنۡ ءَامَنَتۡ مِن قَبۡلُ أَوۡ كَسَبَتۡ فِيٓ إِيمَٰنِهَا خَيۡرٗاۗ قُلِ ٱنتَظِرُوٓاْ إِنَّا مُنتَظِرُونَ

Wanangoja jengine ila wawafikie Malaika, au awafikie Mola wako Mlezi, au zifike baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi? Siku zitakapo fika baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi, kuamini hapo hakutomfaa mtu kitu, ikiwa hakuwa ameamini kabla yake, au amefanya kheri katika Imani yake. Sema: Ngojeni, nasi pia tunangoja.

Explanation & meanings · 1
  1. Hoja imekwisha simama ya kuwa kuamini ni waajibu. Na watu hawa hawakuamini. Basi wanangojea nini ndio waamini? Je, wanangojea wawajie Malaika wawe ni Mitume badala ya kuwa wanaadamu, au wawe ni mashahidi kushuhudia ukweli wako? Au aje Mwenyewe Mola wako Mlezi, wamwone, au ashuhudie ukweli wako? Au zije baadhi ya alama za Mola wako Mlezi zishuhudie ukweli wako? Na pindi zikija hizo alama za Mola wako Mlezi za kuwapelekea kuamini, basi Imani yao haitowafaa kitu. Kwani hiyo itakuwa ni Imani ya kahari, hawana hila. Na sasa tena haimfalii mwenye kuasi toba yake na ut'iifu wake. Kiwango cha kufanya waajibu kimekwisha pita! Waambie hawa wanao kataa na kukanusha: Ngojeni moja ya mambo hayo matatu, nanyi endeleeni katika kukanusha kwenu. Nasi pia tunangoja hukumu ya Mwenyezi Mungu juu yenu.