Skip to content
الأنعَام /

Aya 136

6 : 136

Aya 136 of الأنعَام (6 : 136). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأنعَام Aya 165
Sura · الأنعَام
Kiswahili · Barawani
6 : 136

وَجَعَلُواْ لِلَّهِ مِمَّا ذَرَأَ مِنَ ٱلۡحَرۡثِ وَٱلۡأَنۡعَٰمِ نَصِيبٗا فَقَالُواْ هَٰذَا لِلَّهِ بِزَعۡمِهِمۡ وَهَٰذَا لِشُرَكَآئِنَاۖ فَمَا كَانَ لِشُرَكَآئِهِمۡ فَلَا يَصِلُ إِلَى ٱللَّهِۖ وَمَا كَانَ لِلَّهِ فَهُوَ يَصِلُ إِلَىٰ شُرَكَآئِهِمۡۗ سَآءَ مَا يَحۡكُمُونَ

Na wamemwekea sehemu Mwenyezi Mungu katika mimea na wanyama alio umba, nao husema: Hii ni sehemu ya Mwenyezi Mungu - kwa madai yao - na hii ni ya miungu tunao washirikisha. Basi vile walivyo wakusudia miungu yao havimfikii Mwenyezi Mungu, na vilivyo kuwa vya Mwenyezi Mungu huwafikia miungu yao. Ni uovu kabisa hayo wanayo yahukumu.

Explanation & meanings · 1
  1. Na washirikina, ambao wanayaabudu masanamu, wamo katika udanganyifu wa daima. Wao hufanya katika aliyo yaumba Mwenyezi Mungu Mtukufu, katika mazao ya mimea, na ngamia, na ng'ombe, na kondoo, fungu la Mwenyezi Mungu Mtukufu wakiwatumilia wageni na wenye haja, na fungu jingine hulitumia katika kuwakhudumia masanamu ambayo wameyafanya ni washirika wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa mujibu wa madai yao! Ama walicho wawekea masanamu huwafikia masanamu yao, na hukitumia kwa ajili yao. Na walicho muwekea Mwenyezi Mungu Mtukufu hakifiki chochote kwa hao wageni na mafakiri! Uovu ulioje huu wa hukumu yao ya dhulma! Kwani wao wameyafanya masanamu ndio wenziwe Mwenye kuumba hiyo mimea na wanyama, na hawatumii inavyo stahiki hicho walicho mwekea Mwenyezi Mungu.