43 : 57
۞ وَلَمَّا ضُرِبَ ٱبۡنُ مَرۡيَمَ مَثَلًا إِذَا قَوۡمُكَ مِنۡهُ يَصِدُّونَ
Na alipo pigiwa mfano Mwana wa Mariamu, watu wako waliupiga ukelele.
Explanation & meanings · 1
- Na alipo pigiwa mfano Isa bin Maryam katika kuwa kwake kama Adam kwa kuwa Mwenyezi Mungu alimuumba kwa udongo, kisha akamwambia: Kuwa, na akawa, subhanallah. Basi yeye ni mtumwa aliye umbwa, aliye neemeshwa kwa kupewa Unabii, subhanallah. Haifai kumuabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Na watu wako wanapuuza hizo sifa zinazo pigiwa mfano, na wala hawafahamu.