Skip to content
النِّسَاء /

Aya 33

4 : 33

Aya 33 of النِّسَاء (4 : 33). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

النِّسَاء Aya 176
Sura · النِّسَاء
Kiswahili · Barawani
4 : 33

وَلِكُلّٖ جَعَلۡنَا مَوَٰلِيَ مِمَّا تَرَكَ ٱلۡوَٰلِدَانِ وَٱلۡأَقۡرَبُونَۚ وَٱلَّذِينَ عَقَدَتۡ أَيۡمَٰنُكُمۡ فَـَٔاتُوهُمۡ نَصِيبَهُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدًا

Na kila mmoja tumemwekea warithi katika waliyo yaacha wazazi wawili na jamaa. Na mlio fungamana nao ahadi wapeni fungu lao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa kila kitu.

Explanation & meanings · 1
  1. Na wote, wanaume na wanawake, tumewajaalia kuwa wanastahiki urithi wao wa kuwarithi wazazi wawili, na jamaa, na wale ambao mfiliwa amefungamana nao kwa agano ambalo matokeo yake ni kuwa amrithi ijapokuwa si jamaa, na amsaidie pindi anahitajia msaada kuwa ni badala yake. Basi mpeni haki yake kila mwenye haki, wala msipunguze kitu. Hakika Mwenyezi Mungu anakuangalieni kwa kila kitu, na yuko pamoja nanyi, anashuhudia yote myafanyayo.