Skip to content
النِّسَاء /

Aya 28

4 : 28

Aya 28 of النِّسَاء (4 : 28). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

النِّسَاء Aya 176
Sura · النِّسَاء
Kiswahili · Barawani
4 : 28

يُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُخَفِّفَ عَنكُمۡۚ وَخُلِقَ ٱلۡإِنسَٰنُ ضَعِيفٗا

Mwenyezi Mungu anataka kukupunguzieni taabu, na mwanaadamu ameumbwa dhaifu.

Explanation & meanings · 1
  1. Mwenyezi Mungu anataka kukufanyieni wepesi katika kutunga sharia ambazo ndani yake zina sahala na takhfifu kwenu. Kwani hakika Mwenyezi Mungu amemuumba mwanaadamu kiumbe dhaifu katika kupambana na matamanio na maelekeo ya nafsi. Kwa hivyo yanayo mlazimu katika sharia yana wepesi na wasaa. Na hayo kwa fadhila yake na taisiri yake Mwenyezi Mungu ndiyo anayo walazimisha waja wake.